MAMILIONI YA PESA ALIYOINGIZA DIAMOND KWENYE SHOW ZA MWEZI ULIOPITA ....
Staa wa Kesho, Diamond ameendelea kupiga hela kwa show nyingi zinazomfuata kila kukicha. Wingi wa show hizi unazidi kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa Tanzania wenye pesa nyingi zaidi. Tumejaribu kuangalia baadhi ya show alizofanya mwezi huu, atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi ujao ili kukadiria ni kiasi gani anaweza kuwa ameingiza. Baadhi ya show tunafahamu ni kiasi gani aliingiza huku zingine tukikadiria kutokana na jinsi anavyochaji. Show ya nchini Comoro 22 June Katika show hii alisema alilipwa si chini ya dola 25,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 38. Show za Usiku wa wasafi Tabora 28 na 29 June Mara nyingi katika show za ndani Diamond hachukui si chini ya shilingi milioni 10 kwa show mbili huenda akawa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 15. Show ya Tigo Mwanza 30 June Katika show za makampuni kama hizi Diamond hulipwa si chini ya shilingi milioni 10. Kili Music Tour 2013...