Linah alala na Wizkid hotelini
Mwanamuziki wa Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’. Stori: Musa Mateja, Wikienda Dar es Salaam: Imefichuka! Hatimaye ishu ya wanamuziki wa Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’, kudaiwa kulala kitanda kimoja na msanii wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, imebumburuka. Baada ya kuandamwa na skendo hiyo ya kutoka kimapenzi na Wizkid huku mashabiki wake waliyo wengi wakishindwa kuamini juu ya uhusiano huo, hatimaye sasa mambo yamevuja na kujidhihirisha kuwa kweli staa huyo alilala hotelini tena kitanda kimoja na Mnigeria huyo. Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’. Kikieleza kwa kujiamini, kiliweka wazi kuwa Linah alilala kitanda kimoja na staa huyo kwenye hoteli moja iliyopo Masaki, Dar, baada ya msanii huyo kutua Bongo kwa ajili ya kufanya makamuzi kwenye moja ya shoo zake alizokuwa ameletwa na promota King Solomon. “Linah alilala na Wizkid, alikaa naye hadi siku anaondoka kulelekea Nigeria, na nikwambie ukweli uliyojificha ni kwamba, Linah ku...