Tiko Apania Kuifunika Chura
Stori: Gladness Mallya S TAA wa filamu na Bongo Fleva, Tiko Hassan amepania kutengeneza video kali itakayoifunika ile ya Chura ya msanii Snura Mushi iliyopigwa marufuku kuoneshwa. Akichonga na Risasi Vibes, Tiko alisema anaandaa video kali ya wimbo wake wa Watu ambayo ndani yake kutakuwa na kukata mauno ya kufa mtu kuliko ile ya Snura. āItakuwa ni video ambayo haijawahi kutengenezwa hapa Bongo, ni hatari yaani, ninachowaomba mashabiki ni kuisubiri kwani āsoonā itashuka,ā alisema msanii huyo na kuongeza kuwa hata hivyo, haitakuwa iliyokosa maadili.