Posts

Showing posts from May 26, 2016

Aunt: sasa natafuta mapacha

Image
  Aunt Ezekiel akiwa na Mose Iyoyo sambamba na mtoto wao, Cookie STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa baada ya mtoto wake, Cookie kutimiza mwaka, sasa anafanya mpango kutafuta njia ya kupata watoto mapacha ili atulie. Akizungumza na Amani Aunt ambaye amezaa na dansa wa staa wa Bongo Fleva, Diamond, Moze Iyobo alisema kuwa,  anamshukuru Mungu kumpa mtoto ambaye amemfungulia njia lakini kwa sasa anatamani mapacha ili awe na jumla ya watoto watatu kisha ndiyo apumzike aendelee na mambo mengine. “Baada ya Cookie kunifungulia jina la kuwa mama sasa nataka niongeze uzao mmoja wa pacha ili niwe na watatu kisha nitapumzika,” alisema Aunt.

RAIS MAGUFULI AONGOZWA KUPIGWA JUJU,VIGOGO WAHAHA KILA KUKICHA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ Mwandishi wetu, Amani DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’, huenda ndiye mtu anayeongoza kwa kupigwa juju kwa waganga wa kienyeji kuliko mtu yeyote nchini kwa sasa,   Amani   linakuja na ushuhuda. Sangoma mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shark Abdullah ‘Kishapu’, akipiga simu kutoka jijini Tanga mwanzoni mwa wiki hii, aliliambia gazeti hili kuwa katika miezi ya hivi karibuni, amekuwa akipata wateja, wakiwemo wafanyabiashara na watumishi wa umma wakimtaka kumpunguza kasi ya utendaji kiongozi huyo, wakisema inawaathiri. “Sikiliza ndugu mwandishi, mimi hapa ni mganga wa kienyeji, nataka nikupe habari. Kuna watu wengi sana wanakuja hapa kwangu kutaka niwakinge na tumbuatumbua ya Magufuli, wengine wanataka nifanye ninavyoweza kumfanya asiweze kutekeleza majukumu yake. “Nimewapokea wafanyabiashara na hata viongozi wakubwa, wanataka utumb...