MAJI YA MOTO YALIVYO NA FAIDA MWILINI
KUNA tiba nyingi za kitabibu zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa. Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, maji moto yanatibu magonjwa mengi ikiwemo figo, kutoa sumu mwilini na kuyeyusha mafuta tumboni. Pia hurahisisha mzunguko wa damu, huondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo. Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku unywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia jasho. Wataalamu wa afya wanasema kuwa ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima. Mwinyimvua Pazi, Mtaalamu wa Chakula na Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula