Posts

Showing posts from November 7, 2016

Makonda Kujenga Vituo 20 Vya Kisasa Vya Polisi Dar

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi Kituo cha Polisi cha Tandika, Dar. ..Maongezi yakiendelea katika Kituo cha Polisi cha Tandika. Makonda akizungumza na mmoja wa mahabusu alipotembelea vituo vya polisi.   Kituo cha Polisi Kigogo, Dar. Muonekano wa Kituo cha Polisi Traffic Mwenge, Dar. Tangu kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi na taarifa za changamoto zifuatazo kuhusu hali ya huduma za kipolisi mkoani kwake;- 1. Wananchi kutokupatiwa huduma kwa saa 24 kutokana na vituo hivyo kufungwa usiku. 2. Mazingira mabovu na yasiyoridhisha ya vituo vya polisi. 3. Polisi kutofika kwenye matukio kwa wakati pindi wapigiwapo simu na wananchi. 4. Polisi kushindwa kutoa huduma kutokana na upungufu wa askari polisi. 5. Majambazi kuvamia vituo vya polisi wakiwa na lengo la kuchukua silaha. Changamoto hizi za msingi na ambazo zinahatarisha uhakika wa usalama wa raia wa Dar es

ALICHO ANDIKA MBUNGE TUNDU LISSU KUHUSU KIFO CHA SAMMUEL SITTA

Image

YANAYOENDELEA KUJIRI NYUMBANI KWA MAREHEMU SAMUEL SITTA

Image
 Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akisaini kitabu cha maombolezo, wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Msiba upo Nyumbani kwa Marehemu, Masaki jijini Dar es salaam.  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na baadhi ya viongozi pamoja ndugu wa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akisaini kitabu cha Maombolezo cha aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Sehemu ya ndugu wa Marehemu wakiwa nyumbani hapo.

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Samwel Sitta samwel-sittaaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo lililopo Mkoani Tabora Mhe. Samwel Sitta. Mhe. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita. Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samwel Sitta na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo. “Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali. “Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia nzima ya marehemu, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu” amesema Rais Magufuli katika salamu hizo. Dkt. Magufuli amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na amewaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu. “Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Ameni” Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam 07 Novemba, 2016

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo lililopo Mkoani Tabora Mhe. Samwel Sitta.   Mhe. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.   Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samwel Sitta na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.   “Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.   “Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimb

Tanzia: Spika Samwel Sitta Afariki Dunia

Image
  DAR ES SALAAM : Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani. Mtoto wa marehemu, Benjamin Sitta amesema baba yake amefariki saa 10:00 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani. ‘’Nikweli mzee amefariki nchini Ujerumani akiwa anapatiwa matibabu, alipelekwa Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbulia na saratani ya tezi dume ambayo ilisambaa na kuathiri miguu na mwili mzima. Benjamin amesema kuwa taarifa za mipango ya kusafirisha mwili zitatolewa baadaye. Sitta aliyezaliwa Desemba 18, 1942, alikuwa Spika wa Bunge tangu mwaka 2005 baada ya kustaafu kwa aliyekuwa spika wa Bunge hilo, Pius Msekwa, hadi mwaka 2010 na pia Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Tabora. Mwaka 2010, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki cheo alichokitumikia hadi hadi mwaka 201

Afrima Awards: Diamond Platnumz Anyakua Tuzo 3

Image
Lagos, Nigeria: Diamond Platnumz ameibuka na ushindi wa nguvu kwenye tuzo za Afrima 2016 zilizotolewa Jumapili hii jijini Lagos, Nigeria. Muimbaji huyo ameshinda tuzo tatu, Song of The Year – Utanipenda, Best Artist/Duo/Song Of The Year Utanipenda na Best Male Artist in Eastern Africa. Pamoja na ushindi huo, Diamond pia alitumbuiza wimbo alioimba na Papa Wemba, msanii aliyetunukiwa tuzo ya heshima. Wasanii wengine waliotumbuiza ni pamoja na Patoranking, P-Square, Falz, Eddy Kenzo, Avril, Simi, Darey, Phyno, Seyi Shay na wengine. Chini ni orodha ya washindi kwenye tuzo hizo pamoja na picha za ndani ya ukumbi na red carpet: Artist of the Year  Wizkid Song of The Year Utanipenda – Diamond Album of the Year Ahmed Soultan Revelation of the year Falz Video of the Year Dogo Yaro – Vvip Best African Collaboration Eddy Kenzo ft Niniola – Mbilo Mbilo (Remix) Best African Group VVip Best African Jazz Jimmy Dludlu Best Artist/Duo/Song Of The Year  Diamond –