Angalia Picha Mwanamke Tajiri Zaidi Duniani kwa Sasa, Aliyechukua Mikoba ya Liliane Bettencourt
Baada ya Mfaransa Liliane Bettencourt, 94, kufariki mwezi uliopita, ambaye alikuwa mmiliki wa maduka ya bidhaa za urembo L’Oreal, ambaye ndiye aliyekuwa mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 39.5, sawa na takriban Tshs trilioni 94, mikoba yake imepata mrithi. Mikoba hiyo imechukuliwa na Alice Walton, ambaye ana mali ya jumla ya Dola za Marekani bilioni 33.8. Kwa jumla, alishikilia nambari 17 katika orodha ya mabilionea wa Forbes waliotangazwa mapema mwaka huu. Hadi kufikia mwezi November mwaka huu Alice Walton ametajwa kuwa na utajiri wa Dola bilioni 45.9 sawa na Tsh za Tanzania trilioni 108. Watson ambaye ni binti pekee wa mwanzilishi wa maduka ya Wal-Mart Sam Walton, ndiye mwanamke tajiri zaidi Marekani na utajiri wake unatokana na hisa zake katika Wal-Mart pamoja na malipo ya mgawo wa faida.