THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulucommpress@googlemail.com Website : www.ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425 PRESIDENT’S OFFICE, STATE HOUSE, 1 BARACK OBAMA ROAD, 11400 DAR ES SALAAM. Tanzania. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, kuanzia leo, Jumatatu, Mei 25, 2015. Aidha, Rais Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini. Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole Lenga kutoka Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict Kulikela Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili ...