Posts

Showing posts from October 9, 2013

Mzee Majuto atangaza kujitosa kugombea ubunge mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM

Image
Kwa mujibu wa mtandao wa Bongomovies, msanii mkongwe wa vichekesho hapa nchini, Amri Athumani 'King Majuto' ametangaza kugombea ubunge katika jimbo la Tanga Mjini mwaka 2015 Majuto mwenye umri zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds na amedai kwamba atagombea kupitia CCM. Juhudi za kumtafuta mzee Majuto ili aweze kututhibitishia kama habari hizi ni za kweli au la na kama ni kweli ana mipango gani na jimbo hilo la Tanga mjini zinafanyika...

UDOM yashindwa kudahili wanafunzi wengi kutokana na wanafunzi hao kutokuwa na VIGEZO

Image
CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimeshindwa kudahili wanafunzi wa kutosha kutokana na wahitimu kutokuwa na vigezo. Malengo ya kuanzishwa kwa chuo hicho ni kudahili wanafunzi 40,000 ifikapo mwaka 2015 lakini hadi sasa idadi ya wanafunzi waliopo hawazidi 15,000. Taarifa hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula wakati wa uzinduzi wa baraza la pili la wafanyakazi la chuo hicho. Profesa Kikula alisema idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa chuoni hapo inaendelea kushuka siku hadi siku ikilinganishwa na nafasi zilizopo. "Changamoto zinazotukabili ni nyingi lakini za msingi ni idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa imendeelea kushuka mwaka hadi mwaka kutokana na ukosefu wa wahitimu wa kutosha wenye vigezo vya kudahiliwa katika kozi zetu. "Changamoto nyingine ni ufinyu wa bajeti unaotokana na vyanzo vichache vya mapato ya chuo na pia ufinyu wa ruzuku ya Serikali ndiyo vinakwamisha chuo kufikia malengo yake kama ilivyotara...

Hiki ni KILIO cha msanii DIAMOND baada ya kufanyiwa UMAFIA na Producer wake

Image
Hii ni kauli ya uchungu ya msanii Diamond ambaye analaani kitendo cha producer wake kuuvujisha wimbo wake mpya wa Nikifa Kesho: "Kuvujisha Nyimbo yangu hakuwezi kunipunguzia wala Kunidhuru chochote… Sanasana utanizidishia Umaarufu na kunipa Show zaidi… " Kama nimeacha kurecord nyimbo Studio kwako Uspanick, Relax.. tafta Msanii mwingine Mkali zaidi yangu umrecordie Ngoma Ahit kushinda mimi… .ila Kuvujisha Unajisumbua bure" – Diamond "Hisia zangu zapelekea kuandika haya nikiwa na uzuni ndani yake kwa kuwa muda nilioutmia na akili nliotumia dhairi ni Mungu Pekee anajua ndio Maana aina budi namwachia Mungu pia…. "Imani iliyo ndani yangu nikiamini kuwa kutoa ya Moyoni uufanya Moyo kujengeka Upya, Mwenyezi Mungu Atanijenga Upya na kuwaandalia kitu kipya hivI karibuni"– Diamond "Hii ni changamoto kwangu na Kuweza kujua sheria za Muziki wangu na kusimamia Haki zangu'