Posts

Showing posts from July 4, 2016

Kitwanga Arejea Jimboni Kwake, Akutana na Wanahabari

Image
Mbunge wa Jimbo la Misungwi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Kitwanga. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Kitwanga leo amekutana na wanahabari nyumbani kwake Misungwi mkoani Mwanza ambapo amesema amerejea jimboni kuwatumikia wananchi. Kitwanga (kulia) wakati akimkabidhi ofisi Mhe. Mwigulu Nchemba. Uteuzi wa Kitwanga ulitenguliwa na  Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli Mei 20 mwaka huu baada ya kuingia bungeni na kujibu swali linalohusu wizara yake akiwa amelewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.