Aveva Amuandikia Barua Rais Magufuli Ya Kuomba Radhi
Rais wa timu ya Simba, Evans Aveva. UONGOZI wa Klabu ya Simba umemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, ukiomba radhi kwa kitendo cha mashabiki wao kufanya uharibifu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Wakati barua hiyo ikiwasilishwa serikalini, upande wa pili Simba chini ya rais wake, Evans Aveva, imeteua kamati maalum ya wajumbe wenye uwezo mzuri wa kifedha kwa ajili ya kuiwezesha kufanya vizuri msimu huu, kamati ambayo ilianza kazi kuanzia katika mechi dhidi ya Yanga. Sehemu ya viti vilivyog’olewa na mashabiki wa Simba siku ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga. Kabla hujaijua kamati hiyo, upande wa kuomba radhi ni kuwa hatua hiyo imefikiwa siku chache tangu serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwakilishwa na waziri wake, Nape Nnauye kuzisimamisha Simba na Yanga kuutumia uwanja huo baada ya uharibifu kutokea wakati wa mechi baina ya timu hizo, Jumamosi iliyopita. Rais wa Jamhuri ya M...