Posts

Showing posts from May 6, 2017

TANESCO Wakata Umeme Kambi ya JWTZ , Magereza na Polisi.......Ofisi ya Mkuu wa Mkoa nayo Nusura Ikatiwe

Image
Agizo la Rais Dk. John Magufuli la kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuzikatia umeme taasisi za Serikali zinazodaiwa jumla ya Sh bilioni 8.6 limeanza kufanya kazi mkoani  Arusha. Ofisi zilizoanza kuonja machungu ya kukosa umeme kuanzia jana hadi zitakapolipa madeni ni Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Oljoro, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Magereza, Hospitali za Serikali na Taasisi za Maji. Nyingine zilizokatiwa umeme ni Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ikiwamo Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha na Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha. Wakati ofisi hizo zikikosa umeme, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ilinusurika baada ya kuanza kulipia deni lake la Sh milioni sita 6 kwa awamu. Akithibitisha kufanyika kwa operesheni hiyo iliyotajwa kuwa endelevu kwa ofisi hizo mkoa mzima, Ofisa Uhusiano wa Tanesco mkoani hapa, Saidy Mremi, alisema inalenga kukusanya madeni yote ya miaka iliyopita. “Tunatekeleza agizo ...

Sugu Amvaa ‘Bashite’ Bungeni

Image
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amemshambulia Bashite huku akisema kuwa mtu huyo alipaswa awe mahakamani na sio ofisini kwa madai kuwa amefoji vyeti vya elimu ya sekondari jambo ambalo ni kosa kisheria. Hayo ameyasema leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia hoja kuhusu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Aidha Sugu amemtaka Rapa ROMA Mkatoliki ajitokeze hadharani aeleze wazi kuhusu alivyotekwa na nani alihusika ili jamii ielewe na mamlaka husika iweze kuchukua hatua ikiwemo kuwabaini waliyotekeleza tukio hilo ambalo si la kibinadamu. Sugu aliwageukia wasanii wa Filamu Bongo ambao hivi karibuni waliandama wakipinga uingizwaji holela wa filamu za nje ambazo wanadai zinaporomosha soko la filamu za ndani. Sugu amewataka wasanii hao waache kutumika kisiasa na badala yake wafate misingi ya kazi zao.

Zitto: Tumethibitisha Kampuni ya Boeing wametuuzia ndege ya mwaka 2009

Image
Kwa Mujibu wa Zitto Kabwe ameandika Taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Facebook "Tumeshathibitisha bila mashaka kuwa Kampuni ya Boeing wametuuzia ndege ya mwaka 2009 Kwa bei ya mwaka 2017. Kazi Kwa Watanzania ni kuishinikiza Serikali iseme imelipa kiasi gani? Nukuu kutoka mtaalamu wa ndege na picha ya uthibitisho wa terrible teen hiyo. Ninasikitika Sana kuwa Rais mwenyewe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ndio walikutana na watu wa Boeing kuhusu dili hili. Ina maana Boeing wamemdanganya Rais wetu. Sio sawa hata kidogo "Terrible Teen" LN19 iliondolewa kutoka was 45-12 na itakabidhiwa Air Tanzania itakapokuwa imemalizika mwishoni mwa Mwaka huu "

UMUHIMU MKUBWA WA KOMAMANGA (POMEGRANATE) JUU YA MARADHI YA KANSA

Image
Uchunguzi mpya umeonyesha kwamba, katika tunda la komamanga kuna kemikali zinazozuia kansa ya matiti isitambae mwilini. Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarada la Utafiti la kuzuia Kansa umeonyesha kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins zinazopatikana kwa wingi kwenye komamanga, zinaweza kuzuia kimeng’enyo (enzyme) aina ya aromatase, suala ambalo huzuia kukua kwa Homoni ya estrogen inayopatikana katika kansa ya matiti. Shiuan Chen Kiongozi wa uchunguzi huo amesema kwamba, kemikali hizo hupunguza uzalishwaji wa estrogen, na kusaidia kuzuia seli za kansa ya matiti zisizaliane mwilini, pamoja na tezi la ugonjwa huo lisikue. Aromatase, ni kimeng’enyo ambacho hugeuza Homoni ya androgen kuwa estrogen, na kushambulia kimeng’enyo hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana na kansa za matiti zinazosababishwa na homoni ya etrogen. Huko nyuma pia uchunguzi ulionyesha kwamba tunda la komamanga lina faida kubwa kiafya hasa kwa kuwa na  anti Oxidant nyingi na vitamin mb...

Bunge lafuta maneno kwenye hotuba ya Sugu kabla ya kusomwa

Image
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu ameagiza Hotuba ya Kambi ya Upinzani kuhusu Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ihaririwe na kufuta maneno yote katika kurasa 17. Zungu ametoa uamuzi huo leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu, hata kabla ya bajeti yenyewe kuwakilishwa na Waziri Dk Harrison Mwakyembe. Zungu amesema amezipihitia hotuba zote na kubaini kuwa ile ya upinzani itakayowalishwa na Joseph Mbilinyi 'Sugu' ina masuala yaliyopo mahakamani ambayo yamekwishazuliwa katika bajeti zilizotangulia. Amesema maneno yenye mwelekeo huo yakisomwa atachukua hatua.

Faida ya majani ya mparachichi

Image
Siku chache zilizopita tuliangazia macho katika kuona faida za kula parachichi, ni amani yangu kwamba ulijifunza jambo kubwa sana, hivyo naomba siku ya leo naomba tuangalie faida majani ya mmea wa parachichi katika mwili wa mwadamu. Zifuatazo ni faida ya majani ya mparachichi. Majani ya parachichi humsaidia mwanamke ambaye hupata maumivu wakati wa hedhi. Unachotakiwa kufanya ni; Chukua majani kiasi ya mparachichi, kisha yachemshe kwenye maji lita moja, ukijiridhisha yamekwisha chemka epua kisha yaache yapoe, kisha anza kunywa maji hayo kiasi cha nusu kikombe cha chai, kunywa muda wa asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja utaona mabadiliko. 1. Majani ya mparachichi  husaidia sana kuongeza kiwango cha maziwa kwa kinamama. 2. Unachotakiwa kufanya ni Tatatafuna jani moja la parachichi kila siku, lakini hakikisha jani unalotafuna liwe katika hali ya safi na umeliosha vizuri. 3. Pia majani haya ya mparachichi ni msaada sana katika kutibu majeraha,...

Njia 10 muhimu ukitaka kuondoa sumu mwilini mwako

Image
Mwili wa binadamu unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na kwa namna mbili; kupitia mazingira tunayoishi kama vile viwanda, migodi na maeneo mengine hatarishi ama kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku. Sumu au takamwili,zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibu magonjwa mbalimbali. Mwili huzalisha sumu au takamwili (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako. Hizi ni ishara zinazoweza kuashiria mwili wako umeingiwa na takamwili: -Uchovu sugu -Maumivu ya maungio -Msongamano puani -Kuumwa kichwa kila mara -Tumbo kujaa gesi -Kufunga choo au kupata choo kigumu -Kukosa utulivu -Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi -Pumzi mbaya -Mzunguko wa hedhi usio sawa -Kuishiwa nguvu -Kushindwa kupungua uzito -Kupenda kula k...