RC Mwanza Atoa Saa 24 Kompyuta iliyoibwa ipatikane Ukerewe
Mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongella. Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uaandaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR) Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri. “OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana”, amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo. Akizungumza...