HAWA NDO MASTAA WA KIKE BONGO WANAOJIHESHIMU...
BAADHI ya watu kwenye jamii wamezoea kusikia au kuona wasanii kibao wakifanya mambo ya ajabu na kuwa na skendo za hapa na pale kama kupigana, mapenzi na kuzungumza mambo yasiyofaa lakini leo tunakuletea listi ya mastaa wanaojiheshimu kwa hapa Bongo... SALOME NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’ Ni staa wa kitambo wa filamu za Kibongo. Ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’. Thea amekuwa ni mfano wa kuigwa na kila msanii anayetaka au anayeingia kwenye tasnia ya filamu na jamii kwa jumla. Thea siyo mtu wa skendo kama walivyo wasanii wengine wa kike Bongo. Amedumu kwenye sanaa kwa muda mrefu akianzia Kundi la Sanaa la Kaole wakati wa michezo ya runingani leo, leo amefikia hatua ya kucheza filamu zake mwenyewe japokuwa kumekuwa na malalamiko haonekani sana kama zamani. SUZAN LEWIS ‘NATASHA’ Ni mkongwe wa maigizo ambaye ni mama wa mtoto mmoja. Natasha ni msanii mwenye heshima tele kwenye tasnia ya filamu Bongo ambapo hivi karibuni aliingia kwenye n...