Posts

Showing posts from August 12, 2017

RAIS MAGUFULI AMPONGEZA UHURU KENYATTA BAADA YAKUTANGAZWA MSHINDI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Agosti, 2017 amempongeza Rais Mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta baada ya jana kutangazwa mshindi wa nafasi ya Urais na Tume Huru Ya Uchaguzi Kenya ( IEBC). Tume Huru ya Uchaguzi Kenya ilitangaza Kenyatta kuwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 (54.27%) dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga 6,762,224 (44.74%), kufuatia matokeo hayo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametoa pongezi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.  "Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema"  alisema Rais Magufuli kupitia mtandao wake wa Twitter  Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) ilisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki na kudai kuwa umekuwa ni uchaguzi wa kipekee kwa Kenya kwani watu waliojitokeza kujiandikisha na kupiga kura ni wengi zaidi ukilinganisha na chaguzi zilizofanyika ki

BILIONEA BILL GATES AFUNGUA AKAUNTI YA ISTARAM TANZANIA NA KUANDIKA UJUME HUU

Image
  F

DC amchapa viboko Mzazi kisa gari kupigwa mawe

Image
MKUU wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amemcharaza viboko mzazi wa mmoja wa watoto walioshambulia gari lake kwa mawe na kuvunja kioo cha nyuma jana. Gari hilo lenye namba za usajili STL 669, lilishambuliwa na watoto watatu katika barabara kuu ya Kondoa-Dodoma, kwenye kijiji cha Paranga wilayani Chemba. Kufuatia kupasuliwa kwa kioo hicho, DC alisimamisha gari hilo na kuwakimbiza watoto waliolipiga mawe, hali iliyozua purupushani kwa muda. DC huyo aliwakimbiza watoto hao kwa lengo la kuwakamata na kuwaadhibu lakini hakuweza kuwakamata baada ya kumzidi mbio. Hata hivyo, wananchi walioshuhudia tukio hilo walimtajia DC majina na sehemu wanakoishi watoto hao ili awafuate majumbani kwao. Ndipo mmoja wa wazazi wa watoto waliohusika na shambulio hilo alikutwa nyumbani akiendelea na shughuli zake na alipohojiwa na DC kuhusu malezi ya mtoto wake, aliingia katika majibizano yaliyomkera DC Odunga. "Malezi? Malezi gani unataka kwangu? Mtoto ametoka shule, mimi nitajuaje an

Mbunge wa CCM Atiwa Mbaroni Akidaiwa Kugonga na Kuua Mwanafunzi

Image
Mbunge Daniel Mtuka. Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia Mbunge Manyoni(CCM), Daniel Mtuka (51) kwa tuhuma ya kumgonga kwa gari mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Sukamahela, Salome Paschal (10) na kusababisha kifo chake papo hapo. Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa, debora Magilingimba alisema tukio hilo limetokea jana katika Kijiji cha Sukamahela tarafa ya Kilimatinde Wilaya ya Manyoni. Alisema siku ya tukio mbunge huyo akitokea Dodoma mjini akiwa njiani kurundi jimboni kwake akiendekesha gari lake aina ya Toyota Prado alimgonga mwanafunzi huyo aliyekuwa  akijaribu kuvuka kutoka upande wa kulia kwenda kushoto mwa barabara. Kamanda huyo alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva Mtuka, kushindwa kuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara. “Mtuhumiwa mbunge Mtuka  anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano na baada ya mahojiano, atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili