Mbunge aangua kilio msibani
Mbunge huyo akilia. Stori: Imelda Mtema, UWAZI D AR ES SALAAM: Ukimwona mtu mzima analia, ujue kuna jambo! Mbunge wa Jimbo la Tarime (CCM) kwa miaka mitano (2010-2015), Nyambari Chacha Mariba Nyangwine (40), amejikuta akimwaga machozi kwenye misa ya kuuombea mwili wa aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni yake ya kuchapa vitabu ya Nyambari Nyangwine Publishers, marehemu Edwin Semzaba (pichani). Tukio hilo lilijiri hivi karibuni kwenye Kanisa Katoliki Mlimani jijini Dar ambako mwili huo ulikuwa ukifanyiwa ibada na kuagwa. Wakati Semzaba akikutwa na mauti, Nyambari alikuwa kwenye safari ya kibiashara nchini Brazil ambapo baada ya kupokea taarifa hizo alikatisha shughuli zake nchini humo na kurejea Tanzania kwa mazishi. Akizungumza na Uwazi jijini Dar juzi, Nyambari alisema alilia kwa sababu marehemu alikuwa msaada mkubwa kwake katika biashara ya vitabu. “Mimi nje ya ubunge ni mchapishaji mkubwa wa vitabu. Marehemu alikuwa mkurugenzi kwenye kampuni ya...