Posts

Showing posts from November 15, 2013

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI WA THAILAND

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Thailand Nchini Tanzania Ittiporn Boonpracong,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kusalimiana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Thailand Nchini Tanzania Ittiporn Boonpracong,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Balozi wa Thailand Nchini Tanzania Ittiporn Boonpracong,baada ya mazungumzo yao,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

MASTAA WAENDELEA KUSHIKANA UCHAWI

Image
Uchunguzi wa gazeti hili ndani ya ulimwengu wa mastaa hao ulibaini kwamba, ukiwaacha wale wa Bongo Fleva ambao wamekuwa wakishikana uchawi kila kukicha, kwenye filamu ndiko hakufai. Ilibumburuka kwamba masuala ya kurogana ndiyo yamesababisha filamu za baadhi yao kudoda na kukosa soko. Inaelezwa kwamba mbali na sinema  zao kubuma sokoni pia wamekuwa wakizibiana riziki za tenda kama ilivyokuwa zamani. Elizabeth Michael 'Lulu'. KIVIPI? Kwa mujibu wa ‘mtaalam’ wao mwenye kituo cha kazi huko Yombo-Buza, Dar, wanachokifanya ni kufifisha na kuzimana nyota hivyo kumpotezea mhusika mvuto kwenye jamii. “Unajua kuna mastaa ambao walikuwa na majina makubwa sana lakini siku hizi siyo kama zamani. “Baadhi wanawaroga wenzao kwa kuwasababishia matatizo ya magonjwa au kwenye familia,” alisema mmoja wa wasanii waliokuwa waking’ara zamani lakini siku hizi kafifia huku akimtolea mfano mwigizaji mmoja wa kiume ambaye mkewe aliwahi kumkuta na hirizi. Katika uchunguzi huo, baa...

AUNT, WOLPER, SNURA WAFUNGA MTAA

Image
                                                     Stori: Hamida Hassan Mastaa wa filamu za Kibongo wenye jina kubwa mjini, Aunt Ezekiel, Jacgueline Wolper na Snura Mushi hivi karibuni walitisha kwa kufunga mtaa kutokana na mauno waliyokuwa wakikata mbele za wapiga ngoma wa Kundi la Baikoko, tukio lililojiri Mwananyamala, Dar nyumbani kwa msanii mwenzao Vanitha Omary. Snura Mushi. Wasanii hao waliwashangaza watu jinsi walivyokuwa wakijituma kukata mauno huku Wolper akimtunza mpiga ngoma na kumkatikia kwa staili mbalimbali zikiwemo za chumbani.… ...

MWILI WA DKT. SENGONDO MVUNGI KUWASILI LEO

Image
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili nchini siku ya Leo. Baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam. Aidha, siku ya Kesho, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16, 2013. Aidha, Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba 17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18, 2013. Dkt. Mvungi alifariki jana (Jumanne, Novemba 12,...

WOLPER AANIKA A - Z YA KULICHOMNASISHA KWA DALLAS

Image
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa suala la yeye kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ halikusababishwa na ukata kwani yeye hakufuata fedha kwa mwanaume huyo. Jacqueline Wolper. Akijibu swali la paparazi wetu lililomtaka afunguke kama alifuata mkwanja kwa Dallas, Wolper alisema moyo wake huwa hauna tamaa ya fedha na aliingia katika penzi la Dallas kwa mapenzi aliyokuwa nayo wakati huo na kwa kuwa yaliisha, maisha yanaendelea. Abdallah Mtoro ‘Dallas’. “Sikufuata pesa kwa Dallas, pesa ni pesa na mapenzi ni mapenzi. Kama ni pesa nilikuwa nazo na hata kabla sijawa naye na sasa pia ninazo, waniache,” alisema Wolper.

WOLPER AANIKA A - Z YA KULICHOMNASISHA KWA DALLAS

Image
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa suala la yeye kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ halikusababishwa na ukata kwani yeye hakufuata fedha kwa mwanaume huyo. Jacqueline Wolper. Akijibu swali la paparazi wetu lililomtaka afunguke kama alifuata mkwanja kwa Dallas, Wolper alisema moyo wake huwa hauna tamaa ya fedha na aliingia katika penzi la Dallas kwa mapenzi aliyokuwa nayo wakati huo na kwa kuwa yaliisha, maisha yanaendelea. Abdallah Mtoro ‘Dallas’. “Sikufuata pesa kwa Dallas, pesa ni pesa na mapenzi ni mapenzi. Kama ni pesa nilikuwa nazo na hata kabla sijawa naye na sasa pia ninazo, waniache,” alisema Wolper.

RAIS DKT KIKWETE NCHINI SRI LANKA LEO

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa alipomtembelea kwa mazungumzo kwenye jengo la Temple Trees jijijini Colombo leo Novemba 14, 2013 kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola mwaka huu (CHOGM 2013)  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini  kitabu  cha  wageni nchini  sri Lanka   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa pamoja na  viongozi  mbali  mbali  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa katika mazungumzo yao  leo (picha  zote na Ikulu) Im