Posts

Showing posts from January 14, 2018

Majaliwa amuagiza CAG kuchunguza mfuko wa CDTF

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa kuendeleza zao la Kahawa (CDTF) na amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza mwenendo wa mfuko huo tangu ulipoanzishwa. Majaliwa agizo hilo leo wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao la kahawa alichokiitisha, mjini Dodoma. Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba uundwaji wa mfuko huo si wa kisheria bali ni wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB). Pia aliagiza kufungwa kwa ofisi za CDTF ili kupisha uchunguzi na baada ya CAG kukamilisha uchunguzi na kukabidhi ripoti, kazi zote zilizokuwa zinafanywa na mfuko huo zitafanywa na Bodi ya Kahawa. Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wanavijiji na badala yake kahawa yote itauzwa kwa njia ya minada.

Mbunge Haonga afichua kuwa wabunge wanajiuza

Image
Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe kwa tiketi ya (CHADEMA), Pascal Haonga amefunguka na kusema kuwa baadhi ya wabunge wamekuwa wakijiuza na kununuliwa kwa bei ndogo na kudai yeye hawezi kuwa sehemu ya watu hao ambao wananunuliwa. Haonga amesema hayo alipokuwa akifanya mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo lake la Mbozi na kusema wabunge na wanasiasa ambao wana hama vyama kwa kununuliwa na kujidai wanaunga mkono utendaji wa Rais wana upungufu wa akili. "Mimi siwezi kufanya kama wabunge wengine huko ambao wamekua wakijiuza kwa bei ndogo, mmesikia madiwani wananunuliwa, wabunge wananunuliwa. Hivi inangia akilini kweli wananchi walikuchagua na wengine walichoma nyumba za wengine, wengine waliamua kuchoma na magari, wengine waliamua kuchoma na mahakama, baiskeli na Pikipiki halafu unakuja kusema eti namuunga mtukufu kwa jitihada na kazi anazofanya. Hivi wewe Mbunge utakuwa na akili au matope" alihoji Haonga Mbali na hilo Mbunge huyo amewaeleza wananch...

Maneno ya Uhuru Kenyatta na Odinga baada ya Olunga kuwa Mkenya wa kwanza kufunga Hat-trick

Image
Michael Olunga amekuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi kuu ya Uhispania ~La Liga. Olunga amefunga magoli matatu (Hat-trick) dhidi ya Las Palmas na kuweka rekodi ya kuwa Mkenya wa Kwanza kufunga hat-trick kwenye Laliga. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kuona taarifa hiyo hakukaa kimya kupitkia ukurasa wake wa Facebook akampongeza Michael Olunga kwa kusema “Ongera Michael Olunga kwa kuweka historia kuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi ya Hispania La Liga na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwa klabu ya Girona katika ligi ya Spain” Nae kiongozi wa Muungano wa Upinzania nchini Kenya Raila Odinga amepost katika ukurasa wake wa Twitter kumpongeza Olunga.  

Kumbe bila kuitwa na Waziri tusingejua Gigy ana mimba

Image
Msanii Gigy Money ambaye hivi karibuni ameonekana akiwa mjamzito na kuwashangaza wengi, amesema hakukusudia kuwajulisha watu bali ilikuwa kwa bahati mbaya wamejua Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv pia Gigy Money amewataka watu kumshukuru Naibu Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na Michezo Juliana Shonza kwa kumuita, kwani bila wito huo watu wasingemuona mtaani na kumuona akiwa na ujauzito wake. “Kwanza Mumshukuru yule waziri la sivyo msingeuona, huwa sipendi kabisa kuongelea masuala ya ujauzito wangu ila siku ile ilitokea bahati mbaya watu wakauona, alafu hao wanaosema nimeweka mimba feki ili serikali inionee huruma mi nina undugu na serikali? Kama mtoto anaokotwa basi subirini nami wangu nitamuokota”, amesema gigy Money. Kauli hiyo ya Gigy Money imekuja siku chache baada ya watu kumuona na ujauzito, huku wengine wakidai ameweka mimba feki ili serikali imuonee huruma.

Rais Magufuli ammwagia sifa Kagame

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame atalisaidia bara la Afrika kusonga mbele kimaendeleo kwa kuwa kiongozi huyo anajua matatizo na shida za nchi nyingi za Afrika. Magufuli amesema hayo leo Januari 14, 2018 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mazungumzo yake na Rais Kagame ambayo yamefanyika leo Ikulu na kusema kuwa Kagame ni mwanamapinduzi wa kweli wa Afrika hivyo atakavyokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika atalisaidia bara hilo kusonga mbele zaidi. "Kagame atakapokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) sisi Tanzania tumeipokea hii kwa raha sana kwa sababu tunamfahamu Rais Kagame lakini pia ni jirani yetu mwema sasa Mwenyekiti atakuwa anatoka ndani ya East Africa Community, nimemuakikishia kuwa sisi Tanzania tutampa ushirikiano wa hali ya juu sana katika nafasi hii atakayokwenda kuichukua na nimemthibitishia kutokana na ushawishi wake Afrik...

Pombe Za Johari Ilikuwa Stresi

Image
J OHARI amefunguka kuwa pombe alizokuwa akinywa zilikuwa zikichangiwa na msongo wa mawazo. Johari ameliambia Spoti Xtra kuwa kutokana na ugumu wa kazi za filamu kwa hivi sasa lazima mtu uchanganyikiwe nini kifanyike ili filamu zisife. “Wakati mwingine nilikuwa nakunywa pombe sana kwa ajili ya msongo wa mawazo lakini niliona sio suluhisho kunywa pombe,” alisema Johari.

BAADA YA UBINGWA WA MAPINDUZI CUP, AZAM FC IMECHUKUA MAAMUZI HAYA KUHUSU SURE BOY…

Image
Salum Abubakar ‘Sure Boy’. Azam Fc imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, hiyo ni baada ya kuifunga URA ya Uganda kwa penati 4-3. Awali katika dakika 90 za mchezo huo, timu hizozilitoka suluhu ya 0-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, jana usiku kisiwani Unguja. Baada ya kukabidhiwa ubingwa huo, taarifa kutoka Azam FC zinaeleza kuwa ubingwa huo wameutoa zawadi kwa kiungo wa timu hiyo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, na hii ni baada ya kufiwa na Mama yake mzazi wiki iliyopita wakati akiwa na timu hiyo kwenye harakati za kuwania taji hilo. Hadi Azam FC inatwaa ubingwa, imeweza kucheza jumla ya mechi sita, ikishinda mara tano na kupoteza mmoja huku ikiruhusu nyavu zake kuguswa mara moja tu, na hii ni walipofungwa bao 1-0 dhidi ya URA kabla ya kulipa kisasi kwenye mchezo huo wa fainali. Kikosi hicho kilitarajiwa kuondoka visiwani Zanzibar, asubuhi ya leo Jumapili kurejea jijini Dar es Salaam tayari kabisa kuanza maandalizi ya kuwakabili Majimaji ...

KAULI YA ALBERTO MSANDO KUHUSU SAKATA LA LEMUTUZ LILILOTIKISA MTANDAONI

Image
From @albertomsando -Kaka na rafiki yangu @lemutuz_superbrandtz; Nimetamani sana nikae kimya upambane na ‘msala’ wako mwenyewe. Lakini nimeshindwa. Nimeshindwa kwa sababu naelewa na najua inavyokuwa pale unapopitia unachopitia. I have been there. Niseme kwamba kwa comments zote unaweza sasa kuelewa kiasi cha chuki dhidi yako. Kiasi cha furaha kwa maadui zako. Lakini ndani yake usiache kuona kiasi kidogo cha upendo na huzuni kutoka kwa marafiki zako. Kosa lako ni kuruhusu kile ambacho wengi wanafanya kufika hadharani kwa kuwa karibu na kumpa nafasi aliyefikisha. Hilo ndio kosa lako la kwanza. “Kosa” la pili ni unavyoishi. Umeamua kuishi maisha yako vile ambavyo wewe mwenyewe umechagua. Kuna wengi wanakereka bila hata sababu. Ni maisha yako! Kosa sio ‘kibamia’ au kujifuta ulipotoka kuoga. Wengi sana wana ‘vibamia’ na wanaoga na kujifuta. Wengi wamekutana navyo na wanaishi navyo. Wala hakuna kosa kuwa na kibamia. Utu na heshima yako ni zaidi ya kila kitu. Ni huzuni ...