Posts

Showing posts from May 30, 2018

Mbwana Samatta Afanya Ziara Makka

Image
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, na mchezaji wa timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta (kulia) akiwa msikitini Makka. …Akiwa na mchezaji mwenzake wa timu ya Genk,  Omar Colley. Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta,  anayekipiga katika timu ya Genk ya nchini Ubelgiji baada ya kumaliza msimu wa ligi kuu nchini humo,  ameelekea nchini Saudia Arabia kwa ajili ya kufanya ziara ya kidini huko Makka. Samatta anatarajiwa kurudi Tanzania mwishoni mwa wiki hii kujiandaa na mchezo wa hisani kati yake na mwanamuziki Alikiba katika mchezo wa soka utakaofanyika Juni 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa taifa kati ya Timu Alikiba dhidi ya Timu Samatta.

Kauli Ya Kitila Mkumbo Kuhusu Katibu Mpya wa CCM

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo. Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Bashiru Ally ni mtu sahihi kwa zama za sasa kuwa katibu mkuu wa chama hicho tawala. Jana Halmashauri Kuu, ambayo ni chombo cha pili kwa ukubwa cha CCM ilikutana kwa siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam, na kumpitisha msomi huyo ambaye aliongoza kamati iliyohakiki mali za chama hicho kwa miezi mitano, kuwa katibu mkuu. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Profesa Mkumbo amesema , “katika kipindi ambacho silaha ya siasa ni nguvu ya hoja, weledi, na uimara CCM imepata katibu mkuu sahihi kwa zama sahihi nakutakia mafanikio makubwa komredi Dk Bashiru Ally.” Uteuzi huo umekuja baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kuandika barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.

Kimenuka! Fumanizi la Mwezi Mtukufu Laibua Ndoa Mpya!

Image
Mke wa Sele Gogo, Shani ldd (mwenye dela lenye rangi nyekundu na nyeupe) akiwa na kundi lake nje ya chumba cha Mwajabu, KUNA mambo ya ajabu ya kila aina ambayo hutokea kwa nyakati tofauti, lakini hili lililojiri katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ni kali zaidi. Mke wa mfanyabiashara maarufu wa unga wa sembe mjini hapa, Seleman Husein almaarufu Sele Gogo aliyefahamika kwa jina la Shani Idd, anadaiwa kuzua timbwili zito katika tukio la fumanizi. Timbwili hilo la fumanizi linatajwa kutibua ndoa ya wawili hao kisha kuibua ndoa mpya kati ya Sele Gogo na mwanamke aliyedaiwa kufumwa naye, Mwajabu Juma ambaye baada ya kizaazaa hicho aliamua kufunga naye pingu za maisha. Kwa mujibu wa mashuhuda, fumanizi hilo lililojaza umati lilijiri kwenye chumba cha Mwajabu kilichopo Mtaa wa Makaburi B Kata ya Mji Mpya mjini hapa wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.     Sele Gogo na Mwajabu wakiwa kwenye pozi baada ya kufunga ndoa, ...