Posts

Showing posts from November 13, 2013

UCHEKI MJENGO MPYAAA WA DIAMOND ANAOUPOROMOSHA .. NI KUFURU TUPU

Image
Diamond hivi sasa yupo nchini Nigeria kwa ajili ya video zake mbili akiwa na Iyanya na Davido lakini bado yupo karibu na mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii. Kutana na post hii kutoka kwa Diamond kwenye ukurasa wake wa facebook inayohusisha nyumba yake.

HIVI NDIVYO MSANII WA TAARAB FUNDIKIRA ALIVYOAGWA ... WENGI WAZIMIA MSIBANI

Image
                Mume wa marehemu, Kaisi Musa Kaisi akiwa na uso wa majonzi. Marehemu Nyawana Fundikira enzi za uhai wake. Baba… Mume wa marehemu, Kaisi Musa Kaisi akiwa na uso wa majonzi. Marehemu Nyawana Fundikira enzi za uhai wake. Baba wa marehemu (kulia) akifuta machozi, kushoto ni mtangazaji wa ITV, Hawa akilia kwa uchungu. Waombolezaji waliohudhuria kwenye msiba huo. Ndugu wa marehemu akilia kwa uchungu baada ya mwili kuondolewa na kupelekwa msikitini kuswaliwa. Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye gari baada ya kutolewa katika hospitali ya Mwananyamala ulikokuwa umehifadhiwa. Waombolezaji wakililia kwa uchungu. Mwili wa marehemu ukipelekwa msikitini. LEO vilio vimetawala nyumbani kwa mzee Fundikira maeneo ya kwa Bibinyau, Magomeni, Dar wakati waombolezaji wakiaga mwili wa aliyekuwa mwimbaji na mtangazaji wa kipindi cha taarab ‘Ambaa na Mwambao’ kinac...

WAPIGA DEBE WAGOMBEA ...

Image
Na Dustan Shekidele, Morogoro NI jambo la kusikitisha kweli. Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Komba Faustine Aloyce ambaye ni mpiga debe, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akipigana na mwenzake katikati ya barabara wakigombea shilingi elfu moja waliyopewa kama ujira katika kituo cha daladala kilichopo Kasanga nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumamosi iliyopita kwenye kituo hicho cha daladala zitokazo Mzumbe, Mlali, Mgeta Melela, Doman na Morogoro mjini kilichopo kando kando ya Barabara Kuu ya Morogoro-lringa. Mashuhuda wa tukio hilo walililiambia gazeti hili kwamba Komba na mwenzake huyo aliyefahamika kwa jina moja la Alunaki, waligombea fedha hiyo waliyopewa baada ya kufanya kupiga debe ambapo kila mmoja alidai ilikuwa yake. Wakati wakiendelea kupigana, gari moja lilitokea kwa kasi, Alunaki aliwahi kukimbia lakini bahati mbaya Komba akakanyagwa na kufariki papo hapo. Kabla ya kupigana, inadaiwa wawili hao ...

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA ELIMU

Image
Na Aron Msigwa – MAELEZO,  Dar es salaam. Serikali imewataka wananchi kuzitumia ipasavyo fursa za elimu zinazotolewa kupitia programu mbalimbali za ikiwemo Elimu ya Watu Wazima (EWW) na ile ya Elimu Nje ya Mfumo Rasmi (ENMRA) ili kupunguza tatizo la umasikini, maradhi na ujinga. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Said Meck Sadiki wakati akitoa taarifa kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi yatakayofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Novemba 13, 2013 yakiongozwa na kauli mbiu “Kisomo kwa ajili ya Karne ya 21” Amesema  serikali imeanzisha programu mbalimbali za elimu kuanzia msingi mpaka sekondari kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata fursa hiyo na kuondokana na tatizo Umaskini, maradhi na ujinga na kuwawezesha kujikwamua  kiuchumi, Kijamii, Kisiasa na Kiutamaduni. Ameeleza kuwa mkoa wa Dar es salaam kwa sasa unara...

CHAZ BABA APATA AJALI MBAYA

Image
Na Shakoor Jongo SAD news kutoka Bongo Dansi ni ajali ya pikipiki aliyopata Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake. C haz Baba akiuguza majeraha aliyoyapata. Risasi Vibes lilifunga safari hadi nyumbani kwake Mwananyamala, Dar kumjulia hali ambapo alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita, Ubungo baada ya kugongwa na gari kwa nyuma. “Nilikuwa natokea Kimara, nikiendesha pikipiki yangu. Si unajua tena ile barabara ipo kwenye matengenezo kwa hiyo vizuizi ni vingi njiani. Ghafla nilishangaa pikipiki ikigongwa kwa nyuma, nikaanguka. “Namshukuru Mungu maana mazingira niliyopata ajali ni mabaya sana isitoshe unajua pindi upatapo ajali kuna wengine wanakuja kukusaidia na wengine ni wezi lakini sikuibiwa kitu. “Nimeumia mkono, kiuno, mguu mmoja wa kushoto na maumivu kwa ndani lakini hakuna sehemu niliyovunjika,” alisema Chaz Baba.

HAYA MAJANGAAZZZ ... MAINDA AANIKA ALIVYOICHOMOA MIMBA YA RAY

Image
HILI ndiyo Risasi bwana! Sikia, kama ulikuwa hujui ni kwamba msanii mkongwe katika filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameibuka na kueleza mengi ikiwemo kutoa mimba ya mpenzi wake wa siku nyingi, Vincent Kigosi, tulia hapohapo.   Ruth Suka ‘Mainda’. Mbali na uhusiano wao huo uliokuwa ukifanywa siri, Mainda ameeleza… Stori:  Jelard Lucas HILI ndiyo Risasi bwana! Sikia, kama ulikuwa hujui ni kwamba msanii mkongwe katika filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ ameibuka na kueleza mengi ikiwemo kutoa mimba ya mpenzi wake wa siku nyingi, Vincent Kigosi, tulia hapohapo.   Ruth Suka ‘Mainda’. Mbali na uhusiano wao huo uliokuwa ukifanywa siri, Mainda ameeleza kwa machungu jinsi Ray alivyomtesa kwa kumchanganya na wasanii wenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Risasi Mchanganyiko lilipata wasaa wa kufanya naye mahojiano ‘exculusive’ kwa saa moja na dakika tano, wikiendi ili...

MKAPA ATIMIZA MIAKA 75 YA KUZALIWA WAKE

Image
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akipongezwa na Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo jana wakati misa ya jubilei ya miaka 75 ya kuzaliwa kwake. Picha na Fidelis Felix.  Dar es Salaam.Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa jana aliadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa kwake kwa kufanya Ibada ya Misa iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo. Katika ibada hiyo ya shukrani iliyofanyika Kanisa Katoliki la Maria Imakulata, Upanga jijini Dar es Salaam, Mkapa aliwataka Watanzania kumshukuru Mungu kwa kila jambo. “Tunamshukuru Mungu kwa majaliwa aliyoipatia nchi yetu ya Tanzania na tunamwomba azidi kuijalia umoja katika yote tunayofanya na tunayokusudia kuyafanya,” alisema Mkapa. Mkapa pia aliwashukuru waumini wenzake katika kanisa hilo, huku akifichua siri kwamba, Kadinali Pengo alimtaka ahamie Kanisa la Mtakatifu Joseph wakati alipokuwa rais, lakini hakukubali. Kwa upande wake, Kardinali Pengo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kumshukuru ...

PICHA YETU YA LEO

Image

Dk.Sengodo Mvungi aliyevamiwa na kukatwa mapanga afariki dunia

Image
Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.   Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia. Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini TUNAPENDA TOA  POLE KWA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI. BWAna KATOA NA BWANA KATWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE