Mwanzilishi wa Facebook Alivyokutana na Akina Yemi Alade Nigeria
Lagos, Nigeria MWANZILISHI na mmiliki wa mtandao maarufu duniani wa Facebook, Mark Zuckerberg juzi Jumanne alianza ziara yake ya siku mbili nchini Nigeria, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kwa nchi za Afrika, na kukutana watu mbalimbali wakiwemo wasanii maarufu wa uigizaji filamu na muziki nchini humo. Katika ziara hiyo, Zuckerberg aliwasili Lagos Jumanne na kufika kwenye kituo maarufu cha ubunifu wa masuala ya mitandao ya kijamii cha Yaba, kilichopo eneo lijulikanalo kam Silicon Valley. Zuckerberg alifanikiwa kutoa elimu ya biashara na masoko kwa watu waliohudhuria kwenye mkutano wake huku akitanua wigo wa watumiaji wa mitandao anayoimiliki ikiwemo Facebook, Instagram na WhatsApp. Baada ya somo hilo la juzi Jumanne, Zuckerberg jana aliamkia mitaani asubuhi akitembelea vijana kwenye Jiji la Lagos bila ulinzi. Alionekana akikifanya jogging kwenye daraja la Lekki Bridge na vijana. Baadhi ya wasanii wa filoamu na muziki nchini Nigeria jana ni pamoja na Richard M...