Posts

Showing posts from May 14, 2018

TAARIFA RASMI YA MAGEREZA KUHUSU KUACHIWA KWA LULU

Image
Taarifa rasmi ya Jeshi la Magereza kuhusu kuachiwa kwa Muigizaji wa Filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye sasa atatumikia kifungo cha nje kumalizia miaka yake miwili aliyohukumiwa kwa kosa la kumuua Steven Kanumba bila kukusudia.

Shamsa Kamjibu Harmonize, Mumewe Kutembea na Wolper

Image
MSANII wa Filamu nchini, Shamsa Ford, amefunguka kuhusu mumewe, Chidi Mapenzi kutajwa na Harmonize kutajwa na Harmonize kwenye orodha ya wanaume waliowahi kutoka kimpenzi na muigizaji mwenzake, Jacqueline Wolper.

BREAKING NEWS: LULU ATOKA GEREZANI .

Image
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imembadilishia adhabu ya kifungo, Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, ambaye kuanzia sasa atatumikia kifungo cha nje. Lulu  Novemba 13 mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake ambaye alikuwa pia mpenzi wake, Steven Charles Kanumba, tukio lililotokea April 7, 2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje, amesema Lulu amebadilishiwa adhabu hiyo kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ambapo atatumikia kifungo cha nje. Amesema pia kwamba, msanii huyo aliachiwa tangu juzi Jumamosi Mei 12, huku akisisitiza kuwa si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, ambayo kisheria inaitwa ‘community service.

Shamsa akiri kuumizwa na Harmonize

Image
Muigizaji wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amekiri kuumizwa na kitendo cha Harmonize kumuhusisha mume wake katika ugomvi wake na ex-girl friend wake, Wolper. Utakumbuka wiki iliyopitia katika kurushiana maneno kati ya Harmonize na Wolper, mume wa Shamsa Ford, Chid Mapenzi alitajwa na Harmonize katika orodha ya wanaume 12 aliodai wametoka kimapenzi na Wolper. Sasa Shamsa amesema si kwa mume wake pekee bali hata mtu wake wa karibu anapozungumzwa kwa ubaya huwa anaumia. “Lazima uumie ukiwa kama binadamu hasa kwa mtu ambaye unampenda sio lazima kwa mume kwa mtu yeyote ambaye unampenda, yupo katika sehemu ya maisha yako lazima ujisikie vibaya,” amesema Shamsa.

Tambua Madhara ya Ulaji wa Chipsi

Image
Chips ni aina ya chakula ambacho hupendwa na watu wengi na pia ni miongoni mwa vyakula vyenye mafuta mengi. chips pia inasemekana ni miongoini mwa vyakula ambavyo hupikwa katika joto la juu zaidi ya 300 degree. Chips ni chakula chenye mafuta mengi na mafuta yanapoingia mwilini huenda kuzunguka sehemu ya mwili wa mwanadamu. kama ni mtu ambaye mazoezi pia hufanyi madhara yake ni kupata magonjwa ya moyo. hivi sasa idadi kubwa ya vijana wanaugua magonjwa mengi yanayo sababishwa na mkusanyiko wa mafuta katika miili yao amabayo huchangiwa na kuto kufanya mazoezi madhara yake mafuta kuziba mirija Mafuta yakiliwa sana husababisha kuzidi mwilini. Pia inasadikika mafuta yaliyopo katika chipsi katika sahani moja ya chisi ya moto endapo utaamua kuchuja kuna uwezekano wa kupata nusu glasi ya mafuta ya kupikia. Kwa hali hii ujue ni hatari. Na mwili huwa hatupi kinachofaa, na badala yake kama hakitumiki wakati huo basi huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Ndio maana tunapokula vy...