Posts

Showing posts from March 7, 2018

Kikosi cha Simba dhidi ya Waarabu Leo

Image
KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, tayari ameshakipanga kikosi chake ambacho kitaanza leo Jumatano kwenye mchezo wao dhidi ya Al Masry ya Misri, huku akiwapa jukumu zito la kufunga mabao washambuliaji wake, Emmanuel Okwi na John Bocco. Mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa ni wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika na utaanza majira ya saa 12 jioni, ingawa Lechantre hakufura­hishwa na muda huo uliopangwa na viongozi. Katika mazoezi ya juzi Jumatatu yaliyoanza majira ya saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Boko uliopo jijini Dar, Championi lilimshuhudia Lechantre akipanga kikosi chake kilichoonekana ndicho cha maan­gamizi ambacho kitatumika kum­maliza Mwarabu leo. Katika kikosi hicho ambacho golini yupo Aishi Manula, walinzi wake ni Shomary Kapombe, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Yusuf Mlipili na James Kotei. Kwenye kiungo wapo; Jonas Mkude, Nicholaus Gyan, Shiza Kichuya, Bocco na Okwi. Katika ma­zoezi hayo yaliyomalizika saa 1:30 usiku, kocha huyo...

Mwenyekiti Mtandao wa Wanafunzi Hajulikani Alipo

Image
TAARIFA zilizoenea mchana huu zinadai kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hajulikani alipo tangu jana saa sita usiku. Marafiki za Nondo wamedai alituma ujumbe kwa viongozi wenzake wa TSNP kuwa yuko katika hatari na baada ya kutuma ujumbe huo simu yake ilikuwa ikipokelewa lakini hakuwa akiongea chochote, na baada ya muda alianza kujiondoa kwenye magroup ya WhatsApp. Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa TSNP kuhusu Nondo inasema hajulikani alipo wakiwemo wazazi wake.   Viongozi wa TSNP wamefika Kituo cha Polisi kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na  kutoa taarifa za kupotea kwake. Feb 18, 2018, Nondo alijitokeza na kuikosoa mienendo ya Jeshi la Polisi na Waziri wa Mambo ya Ndani, na mara ya mwisho kuongea na wanahabari, alishinikiza Waziri  Mwigulu Nchemba ajiuzulu. Hivi karibuni ...

TFDA kuzuia soseji kutoka Afrika Kusini zenye bakteria

Image
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema itazuia uingizaji wa soseji kutoka Afrika Kusini zilizobainika kuwa na bakteria aina ya listeria. Uamuzi wa TFDA unatokana na soseji hizo aina ya Polony kubainika kuwa na aina hiyo ya bakteria wanaosababisha ugonjwa wa listeriosis uliosababisha vifo vya watu 180 nchini Afrika Kusini. Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza akizungumza na Mwananchi jana alisema mamlaka hiyo inalifanyia kazi suala hilo ikiwa ni pamoja na kuzuia uingizwaji wa soseji hizo nchini, “Tunalifanyia kazi kwa kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama soseji husika zipo katika soko,” alisema. Soseji hizo kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na vyombo kadhaa vya kimataifa zinatengenezwa na kiwanda cha tiger brands unit enterprises na cha RCL foods vyote vya Afrika Kusini. Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi alikaririwa na mitandao ya kijamii akisema ameagiza kuondolewa sokoni soseji hizo, huku akiwashauri wananchi kuacha kula. Mot...

Tanzia:Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma mjini afariki dunia Muhimbili

Image
ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Dkt. Kabourou ambaye alizaliwa Mei 23, 1949, amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CHADEMA) kabla ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma. Aidha, Dkt. Kabourou amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki akiiwakilisha Tanzania kuanzia Juni 05, 2007 hadi Juni 04, 2012. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa sasa wa Kigoma Mjini amesema kwao huo ni msiba mkubwa, na umewaacha na majonzi tele. “Tumeamka asubuhi na habari za kusikitisha kuwa Dkt. Amani Walid Kabourou, Mbunge Mstaafu wa Kigoma Mjini ametangulia mbele ya haki. Hakika ni msiba mkubwa kwetu. Mola ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,” ameandika Zitto.