Posts

Showing posts from June 22, 2014

MWIMBAJI MWINGINE WA KWETU PAZURI APATA MWENZA

Image
Katika shangwe za GK siku ya leo, tunakupa picha chache kutoka Kigali nchini Rwanda, ambako mmoja kati ya waimbaji wa muda mrefu wa kundi la Ambassadors of Christ a.k.a Kwetu Pazuri aitwaye Furaha Sandrine , jumapili iliyopita aliutambulisha rasmi ubavu wake uitwao Ngabo Karangwa Tony katika sherehe ya kulipiwa mahari na kuvishwa pete ya uchumba rasmi iliyofanyika nyumbani kwao maeneo ya Gikondo  jijini Kigali, ambapo harusi inatarajiwa kufanyika tarehe 6/7/2014 katika kanisa la Wasabato la Gisenyi na kufuatiwa na shere ya kuwapongeza itakayofanyika katika pwani ya Lac Kivu beach. Furaha akivishwa pete ya uchumba. Baada ya pete ni  matabasamu tuuu. Pete ikionyeshwa na zawadi mkononi akikamata. Akipokea zawadi kutoka kwa mtarajiwa mumewe. Furaha mwenye Furaha. Furaha akiwa na marafiki zake akiwemo Kelly aliyesimama nyuma, mwimbaji wa Ambassadors.

KAZI IMEANZA, SIMBA SC YASAINI BEKI LA TAIFA STARS MIAKA MITATU...YANGA NA MAGAZETI YAO

Image
KAZI imeanza. Simba SC imesajili mchezaji wa kwanza kabisa kwa ajili ya msimu ujao, ambaye ni chipukizi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Joram Nason Mgeveke. Mchezaji huyo chipukizi pekee kutoka kikosi cha maboresho aliyebaki Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij, amesaini Mkataba wa miaka mitatu leo. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Joram amesaini mjini Iringa na rasmi sasa ni mchezaji wa Simba SC. Kifaa cha kwanza 2014-2015; Joram Mgeveke akipeana mikono na Hans Poppe baada ya kusiani Mkataba wa miaka mitatu na Simba SC. Chini anasaini. “Tuna muda mfupi sana kwa ajili ya kufanya usajili, sasa tuna orodha ya wachezaji waliopendekezwa, kwa hiyo tunaanza kuwapandia ndege kuwafuata na kumalizana nao, ndani na nje ya nchi. Tumeanza na Joram, kwa sababu yuko Taifa Stars ambayo inakwenda kambini Botswana,”alisema Poppe.    Poppe amewahakikishia wana...

MGIMWA ATUMIA USAFIRI WA BAISKELI KUWATEMBELEA WANANCHI

Image
 Mbunge wa  jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa akitumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia wapiga kura wake katika kijiji cha Kivalali kata ya Ifunda baada ya gari lake  kupata pacha  wakati wa zikara hiyo hivyo kulazimika kutafuta baiskeli ili kufika haraka mkutanoni kusikiliza kero za  wananchi wake ,amini ni mbunge wa kwanza mkoa wa Iringa kutumia usafiri kama huu kuwafikia wananchi wake,picha nyingine akisalimianana  wananchi wa kijiji Kivalali (picha na Francis Godwin Blog) Na Francis Godwin, Iringa MBUNGE  wa  jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa amevunja rekodi ya  wabunge wa jimbo hilo na majimbo mengine ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa kuachana na matumizi ya magari ya kifahari na kuamua kutumia usafiri wa Baiskeli kuwatembelea  wapiga kura  wake. Huku wananchi wa kata ya Ifunda na Mgama wakisema kuwa ubunge wa Mgimwa si wa mwaka mmoja ama mitano bali  hadi mwaka 2025 had...

KIINGEREZA KILIVYOWAGOMBANISHA ASKARI POLISI NA ASKARI WA MANISPAA YA MOSHI

Image
Baada ya kuzunguka kwa muda mrefu raia huyu wa kigeni ambaye haikufahamika mara moja anatoka nchi gani aliketi katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi kisha akatoa Mkate huku akiulainisha na Jam na kuanza kula. Alikula Silesi kadhaa lakini alionekana mwingi wa mawazo kila alipotafuna mkate . Baadae akasukumia mkate na Maji ya Kilimanjaro. Akafunga maji yake akayarudisha ndani ya begi lake. Akaendelea kutafuna Mkate. Akamuuliza mtu aliyekuwa jirani yake vipi unahitaji na wewe nikupatie kidogo na hii ilikuwa ni silesi ya mwisho. Baada ya kupita muda mgeni huyo aliamua kuondoka eneo alilokuwa ameketi akipata mkate wake wa kila siku. Ghafla nyuma yake akajitokeza askari wa manispaa ya Moshi (Mwenye t-shirt nyeupe) ambaye ana jukumu la kusimamia maswala ya mazingira. Baada ya kufuatilia kwa kina ,ikagundulika kuwa askari huyo alikuwa anamfuatilia mgeni huyo akitaka kumtia mikononi kwa kosa la kutupa taka ambaz...

KILI TOUR YAFUNIKA MKOANI IRINGA PICHA HIZI HAPA

Image
            Watanga zaji wa EATV,Sam misago na Dullah kwenye stage ya kili tour iringa.                            Snura akiwa kwenye stage ya kili tour.                                 Snura akiwa kwenye jukwa la kili tour mkoani iringa.                                Izo biziness akiwa na rich mavoko wakiwa kwenye back steji                        Msanii wa kike mwasiti akiwa kwenye jukwaa la kili tour mkoani iringa                                                 Mtangazaji wa EATV.Dickson msami akiwa namuhoji rich ma...