WEMA: NISIPOPATA MTOTO NAFUNGA KIZAZI
Wema Abraham Isac Sepetu. Exclusive! Hapo nyuma kumepita matukio mengi yaliyomhusu staa mwenye jina lake kwenye tasnia ya sinema za Kibongo, Wema Abraham Isac Sepetu , lakini mwenyewe hakuwa tayari kufungua kinywa kutoa ufafanuzi na hisia zake. Ni kupitia Ijumaa Wikienda ambalo limethubutu kufanya naye mahojiano maalum ambayo ndani yake alifunguka mambo mazito kuhusu maisha yake ya sasa na kuelezea dhamira yake ya kutaka kufunga kizazi endapo safari hii hatajaliwa kupata mtoto baada ya kupata mpenzi mpya. NYUMBANI UNUNIO Katika mahojiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Wema, Ununio jijini Dar, staa huyo ambaye ni Miss Tanzania 2006/07, aliweka wazi mambo ambayo watu wamekuwa wakiyasema bila mpangilio wala kusikia kauli yake. UNGANA NA WEMA Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Wema? Ni muda mrefu sana mashabiki wako hawajakusikia. Je, ni kwa nini umeamua kuwa kimya kiasi hicho? Wema: Sasa hivi nimebadilisha ratiba nzima ya maisha yangu. Kuna vitu ambavyo ...