Posts

Showing posts from February 8, 2016

UN Yalaani Korea Kaskazini Kurusha Kombora la Masafa Marefu

Image
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani hatua ya Korea Kaskazini kulipua Kombora la masafa marefu. Katika taarifa iliyotolewa baada kikao cha dharura mjini New York imesema baraza limekubaliana kuiwekea nchini hiyo vikwazo vya kiuchumi mapema iwezekanavyo,lakini pia baraza hilo limeilaumu Korea Kaskazini kwa kukiuka maazimio ikiwa ni pamoja na hatua yake ya kulipua bomu la nyuklia mwezi January. Kauli hizo za kuilaani hatua hiyo Korea Kaskazini zimetowa maeneo mbali mbali duniani pamoja na kulaumiwa na dunia Korea Kaskani yenyewe imesema imelipua kombora hilo ili kutuma mitambo ya satellite angani,jambo linalopingwa na mahasimu wake kuwa hiyo ni danganya toto kwani ina nia ya kujaribu kombora angani. Akitoa taarifa ya kulaani hatua hiyo Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ambaye pia ni Balozi wa Venezuela Rafael Ramirez Carreno amesema wanachama wamekubaliana kulaani kile alichosema ukiukwaji Korea Kaskazini wa azimio la Umoja wa Mataifa. Rafael Ra...

Ni vitu vidogo lakini ukivizingatika kila asubuhi utakuwa na furaha siku nzima

Image
Wimbo wa Happy wa Pharrell Williams ulikuwa moja ya nyimbo ninazosikiliza kila ninapo amka asubuhi, kwanini sababu ni siku mpya na nilitaka kuanza na furaha kama jina la nyimbo. Je, wewe unafanya nini cha kwanza unapoamka asubuhi.? Kuna vitu vidogo sana unaweza ukawa unafanya kila siku na ukajisikia mwenye furaha na ukaanza siku yako vizuri Usizime Alarm (kengere). Kuna wakati unahitaji kitu cha kukufanya uamke muda unaopanga wewe asubuhi. Kengere ya simu au saa ya mezani, inapoita wengi wetu sababu ya usingizi mwingi tunaizima na kuendelea na usingizi,  kwa dakika chache,  ila ni vizuri kama ulipanga kuamka muda huo basi na uamke . panga ratiba yako na uizoe. Tafuta Ujumbe wa kukupa moyo. Kuna wakati tunahitaji mtu wa kutuambia tunaweza,weka chumbani kwako ujumbe mzuri wa kukupa moyo kama “You’re the Best” au unaweza ukaingia Google na kutafuta “inspiration quotes” hizi ni nikuu za watu mbalimbali, ambazo unaweza kusoma kila unapo amka uanze na s...

Utafiti umeonesha wanaume wenye vipara ni wanaume wenye mvuto zaidi kimapenzi!

Image
Kuna vitu vingi humvutia mtu inapokuja swala la kumchagua mpenzi, siwezi taja sifa zote, kila mtu anasifa zake na vigezo vyake, ila ngoja tuongelee mvuto wa kipekee unaopatikana kwa wanaume wenye vipara. Nikiongelea vipara naongelea wale walio na vipara asili, achilia mbali wale wanaopenda kunyoa vipara japokuwa kuna baadhi ya sifa hapa wanaweza wakawa nazo pia. Muonekano wa kiume: wanaume wenye vipara wengi huwa na muonekana wa kiume zaidi,muonekano nadhifu  sina maana kama wanaume wengine walio na nywele ndefu ama wastani hawana mvuto lah, nauongelea mvuto zaidi ama mvuto wa kipekee. Ujasiri: wanaume wa aina hii wengi huonekana ni wajasiri kwa muonekano wao tu, hii huwafanya kuwa kivutio kwa wanawake. Wana hisia kali za kimapenzi: daktari kutoka Chuo cha Yale Marekani , James B. Hamilton alisema katika utafiti wake wanaume wengi walio na vipara miili yao huwa inazalisha mbegu nyingi za kiume kuliko wanaume wenye nywele, japokuwa si kwa asilimia 100 ali...

INATIA HURUMA SANA....HUYU MTOTO KAOMBA KUONA NDEGE WAKATI AKISUBIRIA KUFA ...ANAUMWA KANSA NA ANASUBIRI KUFA TU

Image
A child in an ambulance is at kotoka airport , u know why,? He want to see an aeroplane before he dies, yes die , his parents couldn't afford treatment for canc er and he was kept at home till it got worse. Now there is nothing to do and he will die any moment from now but he begged the hospital to make him see a plane before he die. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Simba hatari, yashinda mechi ya sita mfululizo.

Image
Wachezaji wa Simba wakishangilia goli. Johnson James, Shinyanga SIMBA ni hatari! wala huwezi kubisha kwa hilo baada ya kufanikiwa kuichapa Kagera Sugar bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa katika Uwanja wa Kambarage, jana. Simba sasa haijapoteza kwenye michezo yote ambayo imecheza chini ya kocha mpya wa timu hiyo, Jackson Mayanja, ukiwa ndiyo mchezo ambao uliaminika kuwa unaweza kuwa kizuizi kwa timu hiyo ya Msimbazi. Hii imeonyesha kuwa Simba ndiyo timu ambayo inaweza kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa baada ya kucheza michezo sita (ukiwemo wa Kombe la FA) mfululizo na kufanikiwa kushinda yote. Ilianza kwa kuichapa Mtibwa 1-0, JKT Ruvu 2-0, Burkina Faso 3-0 (Kombe la FA), African Sports 4-0, Mgambo 5-1 na mchezo wa jana. Simba ambao awali chini ya kocha Dylan Kerr walionekana kuwa nyanya walijipatia bao lao kupitia kwa Ibrahim Ajib, ambaye alifunga bao safi akipata pasi kutoka kwa Hamis Kiiza. Hata hivyo, Simba walikuwa wanaweza kuibuka na us...