Posts

Showing posts from April 19, 2016

Ndugai awaapisha wabunge wapya mjini Dodoma

Image
  Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozwa na Mpambe wa Bunge kuingia kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma  kuongoza kikao cha kwanza cha  mkutano wa tatu wa Bunge   Aprili 19, 2016. Ruth Owenya akiapa kuwa Mbunge  kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 19, 2016. Ritta Kabati akiapa kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2016.   Spika wa Bunge Job Ndugai  (kulia) akimwapisha  Ritta Kabati kuwa mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma  Aprili 19, 2016.   Spika wa Bunge, Job Ndugai akimwapisha Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu,  Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge  Mjini Dodoma Aprili 10, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Waziri Kiongozi  wa Zanzibar  Mstaafu , Shamsi Vuai Nahodha baada ya kuapishwa kuwa Mbunge, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2016.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa ...

Rais Magufuli Amtumbua Mkurugenzi Jiji la Dar.

Image
Rais John Pombe Magufuli AKIHUTUBIA kwenye uzinduzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam mchana huu, Rais John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bw. Wilson Kabwe kutokana na ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya jiji na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  pesa zaidi ya bilioni 3. Rais Magufuli amechukua uamuzi huo mchana huu wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda alitoa hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo. Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe. AKIHUTUBIA kwenye uzinduzi wa darala la Kigamboni jijini Dar es Salaam mchana huu, Rais John Pombe Magu...

BINTI WA MIAKA 19 AWA GUMZO KWA KUFANYA KAZI YA MOCHWARI.

Image
Sabrina Gharib. PWANI: Sabrina Gharib, binti mwenye miaka 19 anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo kwenye Mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, amekuwa gumzo kwa watu wanaokwenda kuchukua miili ya wapendwa wao hospitalini hapo, Uwazi limeibuka naye. “Tulipokwenda kuchukua mwili wa mpendwa wetu Tumbi, tulisikia watu wakimzungumzia msichana mdogo anayehudumia maiti. Kwanza sikuamini lakini nilimuona na kwa kweli alituhudumia vizuri,” alisema Frida John, mmoja wa waliokwenda kuchukua maiti hospitalini hapo. Katikati ya wiki iliyopita, gazeti hili lilikwenda hospitalini hapo likiwa na kundi zima la Global Tv On Line na kufanya mahojiano naye ambapo Sabrina alisema aliamua kusomea kazi ya kuhudumia maiti badala ya unesi kutokana na kujua kuwa, ajira kwa fani hiyo zipo nje nje. MSIKIE MWENYEWE “Niliamua kusomea kazi hii kwa kujua kuwa ina soko la ajira. Awali nilikuwa msichana pekee darasani. Siku ya kwanza kusoma kwa vitendo katika Hospitali ya Iringa...

OMMY DIMPOZ AFUNGUKA MAZITO KUHUSU ALI KIBA,AELEZA KILA KITU

Image
Alikiba akiwa na Ommy Dimpoz katika pozi Msanii Alikiba amefunguka na kusema msanii Ommy Dimpoz alimsumbua sana ili kufanya naye ‘Collabo’ japo anasema alikuwa anamsumbua kwa namna nzuri na si mbaya kwani lengo lake lilikuwa ni kufanya kazi na yeye. Akiongea na East Africa Radio Alikiba alidai kuwa ilimchukua takribani mwezi mmoja kama si miwili ili kufanya kazi hiyo na Ommy Dimpoz kwani anadai kila alipomuahidi kwenda studio mambo yaliingiliana na kujikuta inakwenda zaidi ya miezi miwili ndipo alipopata nafasi na kwenda studio kukamilisha Collabo hiyo. “Ommy Dimpoz alikuja akaniambia Kaka kuna wimbo fulani nataka tufanye, mimi nikamuuliza wewe si unaimba kwenye band? akaniambia ni kweli ila kwa sasa nataka kutoka mwenyewe nikamwambia sawa. Nikamuuliza wimbo huo umefanya wapi akasema kwa KGT nikamwambia pale ni nyumbani kwangu, hivyo nikapata nafasi kuisikiliza kazi ile na kumwambia wimbo huu unahitaji vitu vya ziada. lakini ilinichukua zaidi ya mwezi kama si miezi miwil...

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMTEUA POLEPOLE KUWA MKUU WA WILAYA YA MUSOMA

Image
Posted by JAFE MALIBENEKE at Monday, April 18, 2016 Email This BlogThis! Share to Twitter

RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI AMTEUA ALLY HAPI KUWA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI

Image

MAJALIWA AWASILI DODOMA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana  (kulia) , Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (Wapili kushoto) na Mbunge wa  Nachingwea, Hassan Masala baada ya kuwasili kwenye uwanja w ndege wa Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiw kuanza Arili 19, 2016.. Watatu kulia  Mbunge wa Bunge  la Afrika ya Mashariki Adam Kimbisa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana  (kulia) , Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (Wapili kushoto) na Mbunge wa  Nachingwea, Hassan Masala baada ya kuwasili kwenye uwanja w ndege wa Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiw kuanza Aprili 19, 2016.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MABADILIKO YA MUDA WA MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI SIKU YA JUMANNE TAREHE 19 APRILI 2016

Image
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa Daraja la Kigamboni kesho, Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016. Kutokana na ufunguzi huo, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu watumiaji barabara na Wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya magari kutumia daraja hilo itafungwa kwa muda kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana ili kuwezesha kufanyika kwa sherehe hiyo ya ufunguzi wa daraja. Aidha, huduma katika Daraja la Kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia saa 8:00. Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi  (approach roads)  upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.  Imetolewa na; Eng. Joseph M. Nyamhanga Katibu Mkuu  (Ujenzi) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na...

KIGOGO WA DAWA ZA KULEVYA HOFU YATANDA SHKUBA KUTOROKA GEREZANI

Image
Ali Khatib Haji ‘Shkuba’. Stori: Hashim Aziz na Makongoro Oging’, UWAZI Kufuatia kuendelea kushikiliwa kwa kigogo anayedaiwa kujishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’, Ali Khatib Haji ‘Shkuba’ (pichani) katika Gereza Kuu la Mkoa wa Lindi, hofu imezidi kutanda kwa madai kwamba, mfanyabiashara huyo yupo kwenye maandalizi ya kutoroka gerezani hapo, Uwazi limechimba kwa kina. BOMBA LA MAJI LATAJWA Habari zilizolifikia gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita na kutiliwa nguvu na hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea gereza hilo, zilieleza kwamba, kuna ‘mchongo’ unaofanywa na vigogo kadhaa wa unga kwa lengo la kumtorosha Shkuba, wakitumia kivuli cha mradi wa kuingiza bomba la maji gerezani hapo ambapo pengine hata wenye mradi huo hawajui lolote. “Kuna bomba linachimbwa kuingia gerezani, wenyewe wanasema ni mradi wa kulipatia gereza hilo maji lakini kuna tetesi kwamba huenda bomba hilo ndiyo njia ya kutaka kumtolea Shkuba gerezani lakini weny...

RAIS MAGUFULI ATINGA BENKI YA CRDB NA GARI BINAFSI

Image
Muuza maji (kushoto) akishangaa gari alilopanda Rais Magufuli leo asubuhi wakati akitoka Benki ya CRDB tawi la Holland. Gari alilokuwa amepanda Rais John Magufuli lenye namba za usaji T 182 DGQ likitoka katika benki ya CRDB tawi la Holland lililopo katika makutano ya barabara ya Samora na Ohio jijini Dar es Salaam. Rais John Magufuli akiwa ndani ya gari lenye namba za usajili T182 DFQ huku akiwapungia mkono watu waliokuwa nje ya Benki ya CRDB tawi la Holland jijini Dar es Salaam jana, wakati akitoka katika benki hiyo. (Picha na Francis Dande) RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezua taharuki mjini leo baada ya kufika katika Tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari binafsi lenye namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya adamu na hawa wala bendera. Tukio hilo lililochukuwa takribani dakika 25, limetokea majira ya saa nne asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam katika tawi la benki hiyo ambalo liko katika makutano ya...

Kova aibuka sakata la Lugumi

Image
Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Stori: Ojuku Abraham, UWAZI DAR ES SALAAM: Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (pichani) ameibuka kufuatia ‘kubumburuka’ kwa sakata linalomhusu mfanyabiashara Said Lugumi, anayemiliki kampuni ya Lugumi Enterprises inayodaiwa kuingia mkataba tata na Jeshi la Polisi Tanzania. Mkataba kati ya Lugumi Enterprises na jeshi hilo ulisainiwa mwaka 2011, ulihusu kufungwa kwa vifaa vya kuchukulia alama za vidole katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya shilingi bilioni 37. Lakini hadi sasa, vifaa hivyo vimefungwa katika vituo 14, vyote vikidaiwa kuwa ni vya Dar es Salaam lakini bila kujulikana sehemu. Kova, ndiye aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam wakati vifaa hivyo vikifungwa katika vituo 11 vya Polisi huku ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi ikiwa chini ya Said Mwema. Kampuni hiyo inadaiwa kulipwa karibu asilimia 99 ya fedha zote za makubaliano. ...