Maswali 6 utajiri wa Sh.bilioni 8 wa Diamond
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz. Hashim Aziz na Musa Mateja, RISASI mchanganyiko Dar es Salaam: Hivi karibuni, Mtandao wa The Net Worth (www.the-net-worth.com) umetangaza utajiri wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ (26) ambapo kwa mujibu wa jarida hilo, nyota huyo ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani (sawa na zaidi ya shilingi bilioni 8.75), jambo lililozua maswali yapatayo 6 miongoni mwa Wabongo. Mtandao huo umekuwa ukijipambanua kwa kuanika utajiri wa watu maarufu barani Afrika wakiwemo David Adedeji Adeleke ‘Davido’ (shilingi bilioni 32), Ayodeji Balogun ‘Wizkid’ (bilioni 24) na wengineo kibao. Baadhi ya wasomaji wa gazeti hili wameuliza maswali hayo wakisema mwenye uwezo wa kuyajibu ni Diamond mwenyewe na si jarida hilo huku wakitia shaka kwamba, huenda waandaaji wa jarida hilio wamepewa taarifa za uongo na Diamond mwenyewe. AMEPATA WAPI UTAJIRI HUO WA HARAKA? Swali la kwanza ambalo wengi waliosikia taarif...