Posts

Showing posts from November 21, 2017

ENGO LA CLOUDS MEDIA GROUP LAUNGUA MOTO

Image
Mafundi umeme na Zimamoto wakiingia kupitia dirishani katika jengo la Clouds Media Group kuzima moto uliounguza baadhi ya ofisi leo jijini Dar es Salaam. …Juhudi za kuingia ndani zikiendelea. Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (wa pili kulia, T-shirt ya bluu) akiwa na askari, wakiangalia juhudi za kuuzima moto uliotokea. …Akiongea na polisi. Wafanyakazi wa Clouds na wananchi wakiwa nje ya jengo lililoshika moto. Muonekano wa Jengo la Clouds Media Group.   Magari ya Zimamoto yaliyofika kupambana na moto huo. SEHEMU  ya jengo la kituo cha Clouds Media Group lililoko Mikocheni jijini Dar es Salaam limeungua moto leo ambapo Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo hicho, Ruge Mutahaba, amesema moto huo ulitokea bila ya mtu yeyote kuwa na taarifa nao ambapo ulianzia katika studio ndogo ya kurekodia. Aliongeza kwamba kituo hicho si mara ya kwanza kupatwa majanga ya moto ambapo mara ya kwanza walipokuwa katika jengo la Kitegauchumi eneo la

Rais Magufuli awaonya Masha na Msando

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli amewaonya wanachama wapya ambao wamehamia ndani ya chama hicho leo kwenye mkutano mkuu wa NEC unaoendelea Ikulu jijini Dar es salaam. Wanachama hao ambao wamehamia na kutangazwa leo ni Mwanasheria Alberto Msando aliyekuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo, Mbunge wa zamani wa Nyamagana Laurent Masha aliyekuwa mwanachama wa Chadema pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema taifa Patrobas Katambi. Wengine ni Profesa Kitila Mkumbo ambaye naye alikuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo pamoja na Sophia Simba ambaye ameomba kurejeshewa uanachama baada ya kufukuzwa kwa muda Akiongea baada ya kuwapokea wanachama hao Rais Magufuli amesema, “Nawaomba msije mkabadilika tena, mmekuja huku na wanachama wamewakubali msirudi tena kule, hiki ni chama cha wote hata watoto watazaliwa watakikuta na watajiunga kwasababu kina misingi imara, kwahiyo msije huku kujaribu”. Rais Magufuli amemaliza kwa kuwapa ruhusa ya kugo

Profesa Kitila, Katambi, Msando waingia CCM

Image
Dar es salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo ametangazwa rasmi leo Jumanne mbele ya mkutano wa NEC, CCM unaoendelea Ikulu jijini Dar es salaam. Mbali na Profesa Kitila ambaye alikuwa kada wa ACT, pia kuna Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Kitambi ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha, Lawrence Masha, Samson Mwigamba na Albert Msando. Akizungumza mbele ya mkutano huo, Profesa Kitila amesema: "Nguvu ya CCM zipo tano, moja ni kwamba ni chama cha watu, ni chama pekee chenye nguvu siyo chama kuogopa watu, tulijaribu huko tulipokuwa lakini yalishindwa." Kwa upande wake, Masha amesema alipoamua kuondoka, baba yake alisikitishwa na uamuzi huo lakini baada ya kutafakari ameamua kurejea nyumbani. Amesema yeye ni mwanaCCM na kijana alilelewa ndani ya chama hicho. "Mwenyekiti wewe ni mfugaji, ng'ombe akiingia zizini amekatwa mkia unamwangalia mara mbili mbili, mimi sijakatwa mkia ni mwaminifu, ukinihitaji nitumie, kudumu Chama cha Mapind

Sophia Simba arudi CCM

Image
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CCM (UWT), Sophia Simba aomba radhi na kuomba kurejea CCM baada ya kufukuzwa uanachama. Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli amesoma barua ya Sophia kuomba radhi mbele ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na kuwahoji wajumbe kama wanakubali kumsamehe jambo lililokubaliwa. "MwanaCCM aliyefukuzwa uanachama amekuwa akiandika barua nyingi za kuomba radhi lakini tumekuwa tukinyamaza,  kikao hiki ndiyo kilimfukuza," amesema Rais Magufuli katika kikao hicho kinachofanyika leo Jumanne. Baada ya kuwahoji wajumbe na kukubaliwa Rais Magufuli aliandika kwenye barua hiyo kuwa amekubaliwa kurudi CCM.

BREAKING : MWANAMKE AFANYIWA UKATILI NA MUMEWE WA KUTISHA KISA KUPATA KAZI,AMWAGIWA TINDIKALI

Image
Mwanamke mmoja kutoka katika wilaya ya Malwani, Mumbai nchini India amejikuta akipata kilema cha kudumu baada ya kumwagiwa tindikali usoni na mumewe siku mbili baada ya kupata ajira serikalini.Zakira Ali SheikhMwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Zakira Ali Sheikh (26) amesema alikatazwa na mumewe ‘Roobab Ali Sheikh’ kutafuta kazi yoyote ya kuajiriwa na kuambiwa kuwa abaki tu nyumbani kwa ajili ya kulea familia na kazi ndogo ndogo. Mwanamke huyo wakati anasimulia kisa hicho kwenye mahojiano yake na gazeti la Hindu Times la nchini India amesema mumewe alikuwa ni fundi magari na alikuwa haachi pesa ya matumizi nyumbani kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza kichwa jinsi ya kuendesha familia yao yenye watoto wawili.Bi. Zakira ambaye tayari jicho lake moja limeshapata upofu amesema alishindwa kuvumilia hali hiyo ndipo alipoamua kupeleka maombi ya kazi kwenye kiwanda cha Serikali cha Sabuni baada ya kuona matangazo ya kazi. Anasema baada ya siku mbili aliona jina lak

ANGALIA PICHA YA KWANZA IRENE UWOYA NA NDUGU ZAKE WALIVYO TEMBELEA KABURI LA MUME WAKE

Image
Familia ya @ireneuwoya8 yafanikiwa kuzulu (kutembelea) kaburi la marehemu NDIKUMANA… mama mdogo na mama uwoya washindwa kujizuia… Wamwaga machozi na kugala Gala juu ya kaburi huku wakihuzunika kupita kiasi… Taarifa zilizo tufikia ni kwamba walinusurika kuzimia kutokana na Pressure iliyosababishwa na kulia sana Post Views: 532