JE! WAJUA KUWA WEWE UNAWEZA KUWA MCHAWI WA MAHUSIANO/MAPENZI YAKO?
WATU wanaamini mno katika uchawi. Wanamaliza fedha kwa waganga wa kienyeji wakiamini kwamba wamerogwa, hivyo wanatafuta ufumbuzi kutoka kwa wataalamu wa mambo ya asili. Wapo wanaoita mambo ya Kiswahili. Kwangu napinga kuita hivyo kwa sababu nami ni Mswahili na kwa uzoefu wangu, sisi Waswahili hatuna utamaduni wa kutegemea mitishamba kuamua hatma za uhusiano wetu wa kimapenzi. Ila baadhi wapo, tena wengi haswaaa! Shika hili kwamba wewe mwenyewe pengine ndiye mchawi wa mapenzi yako. Hujiulizi kwa nini wengine wanadumu? Ni vipi wenzi wengine wanaheshimiana? Inakuaje kwako imekuwa kinyume? Siyo suala la upepo, wakati mwingine ni kujitakia. Kivipi mwenzi wako hakuheshimu? Ni makosa gani ambayo wewe umefanya? Ukishapata majibu ya maswali hayo, utaweza kujua faida za wewe kujitambua. Nakuasa ushike moja kuu kwamba mapenzi ni nidhamu. Yapo kama kioo, ukiyaheshimu nayo yatakuheshimu na utayaona murua. Endapo utayachukulia kwa mzah...