Posts

Showing posts from August 8, 2017

PICHA MATUKIO YANAYOJIRI TAMASHA LA SIMBA Y UWANJA WA TAIFA

Image
Mashabiki wa Simba waliojitokeza kwenye Tamasha la Simba Day linalofanyika Kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salam .. Klabu ya Simba yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam ina utaratibu wake wa kuenzi vitu vyake vya klabu kwa kuanzisha siku maalumu ambayo wanasimba wote hukusanyika pamoja kujadiliana mambo mbalimbali.Agosti 8 ya kila mwaka huwa ndiyo siku hiyo iliyopewa jina la ‘Simba Day’, wameichagua wao Wanasimba kama sehemu ya kumbukumbu ambapo huchagizwa na mambo mengi ikiwemo kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka, kubadilishana mawazo, na mwisho huchezwa mechi ambayo ndiyo huitimisha kila kitu.

UCHAGUZI KENYA: ODINGA, KENYATTA WAPIGA KURA

Image
Kenyatta akipiga kura LEO ni siku ya uchaguzi nchini Kenya na Wakenya wengi wamejitokeza kupiga kura. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 11:00 asubuhi. Mpaka sasa, wagombea wanaochuana vikali, Odinga na Kenyatta, wamepiga kura katika maeneo tofauti. Odinga akipiga kura. Rais Uhuru Kenyatta amepiga kura kwenye shule ya msingi ya Mutomo na amesikika akiwaomba Wakenya wote wafanye uchaguzi huo kwa amani. Kenyatta akipiga kura. Upande mwingine, Odinga amepiga  kura katika  shule ya Kibra, Nairobi. Ikumbukwe kuwa Odinga anagombea kwa mara ya nne sasa.

Rais Museveni Abadilisha Tarehe Yake wa Kuzaliwa

Image
Rais Museveni akikagua nyaraka zake za Ubatizoa. Kwa muda mrefu sana kumekuwa na mijadala hasa katika mitandao ya kijamii nchini Uganda kuhusu umri halisi wa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni. Kwa mara kadhaa serikali ya Uganda imekuwa ikinukuliwa ikisema kwamba Rais Museveni alizaliwa mwaka 1944, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana vyama vya upinzani vilikuwa vikimkosoa Rais Museveni kwamba anadanganya kwa kusema ana miaka 71. Vyama hivyo vilidaiwa kuwa alikuwa na zaidi ya umri wa miaka 75 na asingeweza kugombea tena. …Akiwa na mkewe na viongozi wa kanisa. Lakini mjadala mpya umeibuka ambapo Ikulu ya Uganda imechapisha nyaraka kwenye ukurasa wake wa Facebook zinazoonyesha kwamba nyaraka za ubatizo wa Rais zimeandikwa tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni 3 Agosti 1947 na hivyo sasa ana miaka 70. Kwa minajili hiyo, Rais Museveni atakuwa na umri wa maika 74 wakati Uganda itakapofanya uchaguzi mwingine mwaka 2021 na hivyo ataweza kugombea ten

MREMBO HAMISA MOBETO AJIFUNGUA AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME

Image
Hamisa enzi za ujauzito Mwanamitindo maarufu   ambaye pia ni muuza nyago kunako video za   wasanii Bongo ,   Hamisa Mobbeto, amejifungua mtoto wa kiume leo. Ubuyu wa Hamisa  kujifungua umezagaa mitandaoni baada ya mama yake  mzazi kuposti picha  ya mkono wa mtoto na kuandika maneno yafuatayo. “Alhamdullilah mume wangu miye peke yangu” Baada ya posti hiyo ya  mama yake mzazi , saa chache baadaye Hamisa alithibitisha taarifa hizo kwa kuposti picha ya mtoto wake na kuandika ujumbe ufuatao. “Ahsante Mungu, Karibu duniani mshindi” Hamisa ni mzazi mwenza  wa mfanyabiashara maarufu,  Majizzo , aliyezaa naye mtoto wa kwanza anayeitwa  Fantasy , ambapo mpaka sasa hajaweka wazi ni nani baba wa mtoto wake huyu wa pili.

Umesikia alichokisema Okwi?

Image
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi (katikati mwenye namba 7) akiwa na wachezaji wenzake. KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi amefunguka kuwa amejipanga kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa leo ili kuwathibitishia mashabiki ambao wana hofu na uwezo wake baada ya kushindwa kutamba alipokwenda nchini Denmark kabla ya kurudi kwao Uganda. Okwi aliyetua Simba akitokea SC Villa, ataungana na mastaa wengine wa Simba waliosajiliwa hivi karibuni kuonekana kwa mara ya kwanza wakikichezea kikosi hicho kwenye mchezo waSimba Day mbele ya Wanyarwanda,Rayon Sports. Mshambuliaji huyo ameliambia Championi Jumanne, kuwa atabadilisha mawazo ya mashabiki wengi leo ambao walimuona hana jipya baada ya kushindwa kutamba alipokwenda Denmark kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu dhidi ya Rayon Sports. “Najua mashabiki wengi wana hofu na uwezo wangu kwa sababu muda mrefu umepita baada ya kuondoka hapa Tanzania, lakini niwaambie kwamb

Dokta Avamiwa Usiku, Achinjwa Babati

Image
Dk. Izack Daniel enzi za uhai wake. DUNIA haina huruma! Ndiyo kauli unayoweza kuitoa baada ya hivi karibuni mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Dk. Izack Daniel , mkazi wa Ngarenaro, Babati mkoani Manyara, kukutwa akiwa amechinjwa kama kuku chumbani kwake na watu wasiojulikana. Chanzo makini kililieleza Uwazi kuwa, siku ya tukio, dada wa kazi wa Dokta Izack alitaka kuingia chumbani kwa bosi wake huyo kwa ajili ya kufanya usafi asubuhi. Lakini tofauti na siku nyingine, ilielezwa kuwa, aligonga mlango kwa muda mrefu bila kufunguliwa hivyo aliamua kwenda kugonga dirishani. Ilidaiwa kuwa, hata dirishani nako hakukuwa na majibu ambapo baadaye familia ilipigwa na butwaa baada ya kuona damu zikichuruzika kutoka chumbani hadi sebuleni kupitia chini ya mlango. “Mkewe alikuwa amesafiri hivyo pale nyumbani Dokta Izack alikuwa na wafanyakazi tu na nyumba aliyokuwa amelala ni tofauti na ile wanayolala wafanyakazi. “Siku ya tukio, dada wa kazi alikwenda kwa aji