Posts

Showing posts from December 14, 2014

ZITAMBUE DALILI HATARI ZINAZOASHIRIA KWAMBA UHUSIANO WENU UMEFIKA UKINGONI

Image
1. Kama mwenza wako hakupi kipaumbele katika mambo yanayotokea, pengine anaumwa lakini huambiwi chochote unakuja kusikia hayo kutoka kwa marafiki, anaandika kwenye mitandao ya kijamii, ama ndugu wengine! Anza kuchukua hatua. 2.Kama Wewe/mpenzi wako  anaandaa malengo bila kukushirikisha kuna dalili ya mahusionao yenu kuvunjika kwa sababu malengo ni kwaajili ya baadae na ukiona malengo yako hayamuhusu mwenza wako basi kuna shida. 3.Kama hamna furaha tena kama kipindi kile mlipokuwa mnaanza mapenzi yenu, kama hakuna tena utani na vitu vingine vinavyopelekea furaha baina yenu basi kuna hatari ya mahusiano yanakaribia kuvunjika 4.Unakuwa na furaha zaidi ukiwa na rafiki wa mpenzi wako mnapokuwa mnaongea, kucheza, utani nk kuliko mwenza wako. Au mpenzi wako anafuraha zaidi akiwa na marafiki zako kuliko wewe anza kuwa makini. 5.Kama wazo la kuendelea kuwa pamoja linaondoka kichwani kwako kutokana na sababu moja amanyingine kuna uwezekano wa mahusiano hayo kuelekea mwi...

ZARI NA DIAMOND MAPENZI MOTOMOTO,MAMA DIAMOND AMPOKEA VIZURI MKWE WAKE MPYA ANGALIA PICHA HUKO SOUTH AFRICA

Image
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

SIMBA SC YAICHAPA YANGA 2-0 MTANI JEMBE

Image
Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi akiwatoka mabeki wa Yanga SC, Kevin Yondan aliyelala chini na Juma Abdul  Na BIN ZUBERY SIMBA SC imeendeleza ubabe wake kwa mahasimu wao, Yanga SC katika mechi za Nani Mtani Jembe, baada ya jioni hii kuichapa mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Desemba mwaka jana, Simba iliichapa Yanga SC mabao 3-1 katika mechi ya Mtani Jembe, inayoandaliwa na wadhamini wa timu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro. Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, Simba SC ilikuwa tayari inaongoza kwa mabao hayo mawili, yaliyotiwa kimiani na kiungo Awadh Juma na mshambuliaji Elias Maguri. Awadh Juma alifunga bao la kwanza baada ya kuanzishiwa mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi dakika ya 30, umbali wa mita 23. Elias Maguri aliifungia Simba SC bao la pili dakika ya 42 akimalizia mpira uliorudi baada ya kugonga mwamba kufuatia shuti la Mganda, Simon Sserunkuma. Kiungo wa Yanga SC, Mnyarwand...

MISS WORLD TANZANIA WAZIDI KUANDIKA HISTORIA

Image
Watanzania wameamua kwamba tukiamua tunaweza, good news kutoka London Uingereza, ambako yanafanyika mashindano ya Miss World mwaka 2014. Happiness Watimanywa, mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano hayo ameshare na sisi taarifa nyingine nzuri kupitia ukurasa wake wa Instagram. Happiness kaandika hivi;  “ Hey guys. Siwezi amini kuwa tumefika namba 2. Tuongeze bidii maana nchi nyingine pia wako bize na kura. Lets do this Tanzania!!!! Naamini pamoja tutafika. #votevotevote #PigaKuraSasa#DownloadTheApp#HuuNiMwakaWetu “– @ happinesswatimanywa Zoezi la upigaji wa Kura litasitishwa leo December 14, jioni ambapo Fainali hizo zitakuwa zinafanyika London, Uingereza. Unaweza kuendelea kumpigia kura mshiriki huyo ili arudi na Taji la Miss World 2014.