Posts

Showing posts from April 26, 2017

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA WANANCHI KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO WA TANGANIKA NA ZANZIBAR YENYE KAULI MBIU “MIAKA 53YA MUUNGANO; TUULINDE NA KUUIMARISHA,TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII” APRIL 26,2017

Image
 Amir jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017   Amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipokea heshima na wimbo wa taifa ukipigwa  Amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akilekea kukagua gwaride liloandaliwa na vyombo vya ulizi na usalamaliloandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kusherehekea miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017 Amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride liloandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kusherehekea miaka 53 ya Muungano wa Tanga...

Rais atoa msamaha kwa wafungwa katika kuadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanzania

Image
Katika kuadhimisha Miaka 53 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2017 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:- Wafungwa wote ambao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58, wawe wametumikia nusu (½) ya vifungo vyao vilivyobaki, isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2(i – xxi). Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, Kifua kikuu (TB) na Saratani (Cancer) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa hawa wathibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya. Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi. Umri huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya. Wafungwa wa kike walioingia na mi...

Warembo Washikiana Visu Kisa Penzi la Chuz

Image
WAREMBO wawili wanaofanya tamthiliya ya Closet Chapter, waliofahamika kwa majina moja moja ya Shugga na Kanjo, hivi karibuni walishikiana visu katika ugomvi unaotajwa kuwa ni wa kumgombea bosi wao, Jumanne Kihangala ‘Mr Chuz’. Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho karibu na wasanii hao, sekeseke hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, baada ya Shugga ambaye ni mchumba wa Chuz kumuonya Kanjo apunguze mazoea na mpenzi wake huyo. “Ishu hiyo ilitokea wakati wapo kambini Lushoto wakiwa wanashuti, ndipo Shugga akampiga mkwara Kanjo aache kumshobokea, mwenzake naye akaja juu wakaanza kudundana hadi kushikiana visu, wakidai bora wauane wakose wote, ” kilisema chanzo. Baada ya kupata habari hizo, Za Motomoto News ilimtafuta Mr Chuz  mbaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kusema kinachomponza mchumba wake ni wivu wa kupindukia alionao.

Shuhudia LIVE Makomando Wakionesha matukio ya ujasiri Kwenye Sherehe za Miaka 53 ya Muungano

Image
Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinafanyika leo April 26, 2017 mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, 1964 chini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalim Julius Nyerere na hayati Sheikh Abeid Karume. Kikosi cha makamandoo wakitoa saluti mbele ya Amri Jeshi mkuu katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017 Kikosi cha makomandoo wakionyesha umahili wa mazoezi  mbele ya Amri Jeshi mkuu katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017 Hapa ni kikundi cha Makomando wakionyesha uwezo, Bonyeza play hapa chini kutazama