SPORTS

Kocha wa Yanga Apewa Onyo Kali

KAMATI ya Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) imetoa onyo kali kwa Kocha wa Yanga Luc Eymael kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi yasiyofaa kuhusu ubaguzi wa rangi katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC uliochezwa Januari 18, 2020 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Stephen Mguto amesema kamati hiyo pia imeiomba Yanga kutoa tamko juu ya kauli hizo pamoja na vitendo vingine alivyoeleza kuwa siyo vya kiungwana.

Kuhusu malalamiko ya kocha huyo kuwa alibaguliwa, Mguto amesema alichofanyiwa na mwamuzi Hans Mabena hakikuwa ubaguzi wa rangi.

“Sisi hatukuliona kama ni ubaguzi… Maneno yake aliyosema kwamba amebaguliwa kwa sababu yeye ni mweupe, hayana maana,” amsema Mguto.

...........................................................................................................

WASHINDI WA TUZO ZA MO SIMBA 2018

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz (kushoto) akimpatia Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara.

Tuzo za MO Simba zilizotolewa jana usiku katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  1. GOLIKIPA BORA WA MWAKA
  2. Aishi Manula – WINNER
  3. SaidMohamed ‘Nduda’
  4. Emmanuel Elias Mseja
 BEKI BORA WA MWAKA
  1. Yusuph Mlipili
  2. Erasto Nyoni – WINNER
  3. Shomari Kapombe
  1. KIUNGO BORA WA MWAKA
  2. Jonas Mkude
  3. James Kotei
  4. Shiza Kichuya– WINNER

  1. MSHAMBULIAJI BORA WA MWAKA
  2. Emmanuel Okwi – WINNER
  3. John Bocco
  4. Shiza Kichuya

  1. MCHEZAJI BORA MWANAMKE WA MWAKA
  2. Rukhia Salum
  3. Zainabu Rashidi Pazzi – WINNER
  4. Dotto Makunja

  1. MCHEZAJI BORA MDOGO WA MWAKA
  2. Ally Salim (GK)
  3. Rashid Juma – WINNER
  4. Salumu Shabani

  1. GOLI BORA LA MWAKA
  • John Bocco (Simba VS Mwadui)

  1. TUZO YA BENCHI LA UFUNDI
  2. Pierre Lechantre – Kocha Mkuu
  3. Masoud Djuma – Kocha Msaidizi
  4. Mohamed Aymen – Kocha wa Viungo
  5. Muharam Mohamed – Kipa wa Makipa
  6. Richard Robert – Meneja wa Timu
  7. Yassin Gembe – Daktari wa Timu
  8. Abbas Selemani–Mratibu

  1. SHABIKI BORA WA MWAKA
Fihi Salehe Kambi

  1. MHAMASISHAJI BORA WA MWAKA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
  2. Hamis Mwinjuma (Mwana FA) – WINNER
  3. Salama Jabir –WINNER
  4. Zitto Kabwe
  5. Vyonne Cherrie (Monalisa)
  6. Omary Nyembo (Ommy Dimpoz)

  1. MHAMASISHAJI BORA
– Haji Manara

  1. TAWI BORA LA MWAKA
  2. Wazo Hill
  3. Ubungo Terminal – WINNER
  4. Vuvuzela

  1. KIONGOZI BORA WA MWAKA
         – Kaimu Rais wa klabu ya Simba, Salim Abdallah Muhene

  1. TUZO YA WASIMAMIZI WA MCHAKATO WA MABADILIKO
  2. Jaji Mstaafu Thomasi Mihayo
  3. Wakili Damasi Ndumbaro
  4. Abdulrazak Badru
  5. Mussa Hassan Zungu
  6. Yusuph Nassoro
  7. Brenda Mrema
  8. Mzee Hamis Boma
  9. Revocatus Cosmas Sangu
  10. Hashim Nyendage
  11. Gervas Alpha Honest
  12. Emmanuel Metusela Urembo
  13. Mulamu Nghambi
  14. Selemani Omari
  15. Aziz Kifile
  16. Salim Abdallah Muhene
  17. Arnold Kashembe
  18. Omari Bakari Mtika
  19. Evodius Mtawala

  1. TUZO YA HESHIMA (LIFETIME ACHIEVEMENT)
        – Selemani Matola – WINNER

  • MCHEZAJI BORA WA MWAKA
  1. Emmanuel Okwi
  2. John Bocco – WINNER
  3. Shiza Kichuya

 .........................................................................................................

Hotuba ya Mohammed Dewji Kwenye Tuzo Za Simba


Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji.
MHE MGENI RASMI, DKT. HAMISI KIGWANGALLA, WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,
MHE MGENI MAALUMU, MZEE WETU ALI HASSAN MWINYI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
KAIMU RAIS WA SIMBA,
WAHESHIMIWA VIONGOZI WA SERIKALI,
WAHESHIMIWA WABUNGE,
WAHESHIMIWA MABALOZI,
WAJUMBE WA KAMATI WA UTENDAJI YA KLABU YA SIMBA,
VIONGOZI WA TFF,
VIONGOZI WA BODI YA LIGI,
VIONGOZI WA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA,
WADHAMAINI WA KLABU YA SIMBA,
MWENYEKITI NA WAJUMBE WA KAMATI YA ZABUNI YA KLABU YA SIMBA,
WAJUMBE WA KAMATI YA UWEKEZAJI YA KLABU YA SIMBA,
WANACHAMA WENZANGU,
MARAFIKI ZANGU,
WANAHABARI,
WAGENI WAALIKWA MABIBI NA MABWANA

ASALAAM ALAYKUM.

SIMBA… (NGUVU MOJA)
SIMBA… (NGUVU MOJA)
THIS IS… (SIMBA)

AWALI YA YOTE TUMSHUKURU SANA MWENYEZI MUNGU KWA KUTUWEZESHA KUFIKIA SIKU HII YA LEO. NI SIKU KUBWA SANA KWETU KWENYE SHEREHE HII YA TUZO KWA WATU WALIOI-WEZESHA KLABU YETU YA SIMBA KUFIKA HAPA ILIPO SASA.

KIPEKEE, TUMSHUKURU TENA MWENYEZI MUNGU AMBAYE AMETUWEZESHA KWA MATAKWA YAKE KWA MARA YA KWANZA KUKUTANA BAADA YA KUSHINDA ZABUNI KATIKA KLABU YETU YA SIMBA. NA KUANDAA TUZO AMBAZO ZITAKA-ZOTOLEWAKWA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI, MASHABIKI NA WAPENZI MBALIMBALIWA SIMBA.

NICHUKUE NAFASI HII KUISHUKURU SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA INAYOONGWA NA MHE. RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWA JITIHADA ZA KUSAIDIA NA KUKUZA UCHUMI WETU, AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE, UMETOA FURSA KWETU SISI KUWEZA KUWEKEZA KATIKA MAENEO MBALIMBALI IKIWEPO KATIKA KLABU HII. LAKINI PIA KUWASHUKURU WASAIDIZI WAKE KUANZIA MAKAMU WA RAIS, WAZIRI MKUU NA MAWAZIRI WOTE KWA KAZI KUBWA WANAYOI-FANYA YA KULIJENGA TAIFA HILI.

MHE. MGENI RASMI NA WAGENI WAALIKWA, KAMA MNAVYOFAHAMU KWAMBA KLABU YETU YA SIMBA IMEINGIA KATIKA MFUMO MPYA WA UENDESHAJI AMBAO UMETUPA NAFASI YA KUWEKEZA KATIKA KLABU HII TUNAYOISHABIKIA SANA.

MARA KADHAA NA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI, NIMEKUWA NIKITUMIA SEHEMU YA MUDA WANGU KUJIULIZA? KWANINI MUNGU AMENIFANYA NIWE NA MAPENZI MAKUBWA KIASI HIKI NA KLABU HII.?LAKINI NAAMINI HILI NI JUKUMU AMBALO NIMEPEWA NA MWENYEZI MUNGU ILI NIIFANYIE MAZURI KLABU HII.

KLABU YETU INA HISTORIA KUBWA KATIKA SOKA LA HAPA NCHINI, AFRIKA MASHARIKI, NA AFRIKA KWA UJUMLA, LAKINI HATUKUWA NA UTARATIBU WA KUTOA TUZO KWA WENZETU AMBAO WALIJITOA KWA MOYO WAO WOTE, ILI KUHAKIKISHA TUNAPATA MAFANIKIO KATIKA MICHUANO MBALIMBALI AMBAYO TUNASHIRIKI.

KUNA MASHABIKI WAMEPOTEZA MAISHA YAO KWA AJILI YA SIMBA.KUNA MASHABIKI WANATUMIA SEHEMU KUBWA YA MUDA WAO KWA AJILI YA SIMBA. KUNA VIONGOZI WANAFANYA KAZI KWA BIDII SANA ILI TU. SIMBA IFANIKIWE. KUNA WACHEZAJI WETU WANACHEZA KWA KUJITUMA SANA, ILI SIMBA IPATE MAFANIKIO.KUNA BENCHI LA UFUNDI AMBALO LINAHAKIKISHA LINATUMIA KILA MBINU ILI TU TUPATE MATOKEO MAZURI.

KWA MFANO, TULIKUWA NAYE MCHEZAJI WETU MAREHEMU HUSSEIN TINDWA, AMBAYE ALIFARIKI DUNIA NDANI YA UWANJA, HUKU AKIITUMIKIA KLABU YETUILIPOKUWAIKICHEZA NA MABINGWA WA ZAMANI WA NIGERIA, KLABU YA RACCAH ROVERS MWAKA 1979. HUYU TUNA KILA SABABU YA KUMKUMBUKA,YEYE NA WENGINE KAMA OTHMAN MAMBOSASA, OMARI MAHADHI BIN JABIL, PATRICK MAFISANGO, MOHAMED KAJOLE, ADAMU SABU, EDWARD CHUMILA, MARTIN KIKWA, NA WACHEZAJI WENGINE WENGI WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI. MUNGU AWAREHEMU NA AZILAZE ROHO ZAO MAHALI PEMA PEPONI. AMEEN

KWA RUKHSA YAKO MHE. MGENI RASMI NAOMBA TUSIMAME KWA DAKIKA MOJA ILI TUWAENZINA KUWAKUMBUKA PAMOJA NA KUTOA HESHIMA KWA MALEGENDARIES WETU HAWA.

PAMOJA NA NYOTA WETU HAWA WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI, KLABU YA SIMBA IMETOA NYOTA WENGI SANA KUANZIA KARNE ILIYOPITA MIAKA YA 60 MPAKA HIVI LEO. MIONGONI MWAO NI MBARAKA MOHAMED, ABDALLAH KIBADEN, MTEMI RAMADHANI, ZAMOYONI MOGELA, MALOTA SOMA (BALL JUGGLER), SELEMANI MATOLA NA WENGINE AMBAO HAKUNA ASIYEJUA WALICHOI-FANYIA SIMBA NA TAIFA HILI KWA UJUMLA.

ILINICHUKUA MUDA KUFIKIRIA NI JAMBO GANI TUNAWEZA KUWAFANYIA WENZETU WALIO-ITENDEAMAMBO MAKUBWA KLABU. NA PIA KUWAINSPIRE WACHEZAJI WETU WA SASA, ILI WAWEZE KUJUA THAMANI YA KUCHEZEA SIMBA NA UKUBWA WA KLABU HII. HAPO NDIPO WAZO LA KUTOA TUZO ZA MO SIMBA LILINIJIA. NINAAMINI KWAMBA HII ITAKUWA NI NJIA BORA SANA YA KUTAMBUA MCHANGO WAO AMBAO UMEIWEZESHA SIMBA KUFIKA HAPA BAADA YA MIAKA 81 TANGU KUANZISHWA KWAKE.

HAIKUWA KAZI RAHISI, KWANI BAADA YA KUPATA WAZO LA TUZO NILIKUWA NA KAZI NYINGINE YA KUHAKIKISHA KUNAKUWA NA VIPENGELE AMBAVYO VITAGUSA KILA SEHEMU KWA WATU AMBAO JUHUDI ZAO ZIMESAIDIA SIMBA KUFIKAHAPA, KUANZIA KWA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI, MASHABIKI NA MATAWI YA SIMBA.

ILIKUWA KAZI KWELIKWELI, NA BAADAE NILIPATA VIPENGELE 16 AMBAVYO KWA HAKIKA VITAMGUSA KILA MMOJA WETU KUTOKANA NA JUHUDI ZAKE KWENYE KLABU HII.

ILI KUPATA WASHINDI HALALI, TULIONA NI VYEMA KAZI YA KUCHAGUA WASHINDI NIWAACHIE MASHABIKI WENZANGU AMBAO WALIPATA NAFASI YA KUPIGA KURA KUPITIA TOVUTI YA MOSIMBAAWARDS.CO.TZ NA KURASA ZA SIMBA ZA TWITTER, FACEBOOK NA INSTAGRAM.LAKINI PIA TULITEUA KAMATI AMBAYO ILIHUSISHA WADAU MBALIMBALI WA SOKA HAPA NCHINI KAMA TFF, BODI YA LIGI, MAKOCHA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA, WACHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA, WADHAMINI NA WANAHABARI. NA KATIKA HILI NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HIIKUISHUKURU KAMATI KWA KAZI KUBWA WALIYOIFANYA USIKU NA MCHANA ILI KUHAKIKISHA SHUGHULI HII INAFANIKIWA.

USHINDANI ULIKUWA NI MKUBWA SANA, HIVYO KILA KIPENGELE WALICHAGULIWA WATU WATATU, NA HII HAIMAANISHI KWAMBA AMBAO HAWAKUPATA NAFASI YA KUJUMUISHWA KATIKA VIPENGELE VYA TUZO ZA MWAKA HUU KUWA SIO BORA, BALI ILIKUWA NI LAZIMA KILA KIPENGELE WAPATIKANE WATU WATATU KWA AJILI YA KUPIGIWA KURA.

KWANI KAMA MNAVYOFAHAMU TIMU YETU INA WACHEZAJI WENGI WENYE VIWANGO AMBAVYO HAVIPISHANI SANA. HIVYO USHINDANI ULIKUWA NI MKUBWA, LAKINI MWISHO WA SIKU LAZIMA MSHINDI APATIKANE. BAADHI YA VIPENGELE AMBAVYO VILIKUWA NA USHINDANI MKUBWA NI KIPENGELE CHA MCHEZAJI BORA NA GOLI BORA, KWANI TULITOA NAFASI KWA MASHABIKI WENYEWE NDIO WACHAGUE.

NAOMBA NITUMIE NAFASI HII KUWAOMBA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI NA MASHABIKI, AMBAO WATASHINDA TUZO TUNATEGEMEA KUONA MKIZIDI KUONGEZA JUHUDI ZAIDI ILI KLABU YETU IZIDI KUSONGA MBELE KWA KUPATA MAFANIKIO. NA KWA AMBAO WATAKOSA NIWATIE MOYO KWAMBA HUU SIO MWISHO WA TUZO HIZI. ZITAKUWEPO KILA MWAKA INSHALLAH, HIVYO MKIJITUMA ZAIDI LABDA MWAKANI MNAWEZA KUWA MOJA YA WASHINDI WA TUZO KATIKA VIPENGELE MBALIMBALI AMBAVYO TUTAVIWEKA.

MWISHO, NAPENDA KUWASHUKURU WATU WOTE TULIOWAALIKA KWA KUKUBALI KUITIKIA MWITO WETU. MWENYEZI MUNGU AWAJALIE. MUNGU IBARIKI SIMBA. MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU IBARIKI AFRIKA.

ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA…

THIS IS… (SIMBA)

 

...........................................................................................................

 Himid Mao atua Misri


Baada ya siku moja tu tangu klabu ya Azam FC itangaze kumwacha huru nahodha wake Himid Mao, kiungo huyo ameripotiwa kukamilisha kiporo cha usajili wake ambao ulikwama kwenye dirisha kubwa la Juni 2017 katika klabu ya Petrojet ya Misri.

Akiongea na East Africa Television mapema jana, Himid Mao alithibitisha kuwa anatarajia kuondoka nchini jana jioni kuelekea Afrika Kusini na kisha kuunganisha nchini Misri huku akisisitiza anakwenda kwaajili ya mapumziko lakini ripoti zimeeleza ameshafika Misri na kusaini Petrojet.

Mao ameelezwa kukamilisha uhamisho wake huo kwa kusaini miaka mitatu ya kuichezea timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Misri. Msimu wa 2017/18 Petrojet imemaliza katika nafasi ya 12 ikiwa na alama 38 kwenye mechi 34.

Himid akiwa mwanafunzi wa sekondari alianza kuitumikia  timu ya vijana ya Azam FC mwaka 2011, kabla ya kupata nafasi katika timu kubwa na hatimaye kuaminika zaidi akipata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Azam FC na timu ya taifa Taifa Stars.

Kwa upande wa Uongozi wa Azam FC, umeweka wazi kuwa Himid amefuata taratibu zote za kuondoka klabuni hapo na wao kama timu iliyomlea wamemtakia kila la kheri kwenye soka lake nje ya nchi.

.........................................................................................................

Haji Manara Apewa Onyo Kali na TFF


Msemaji wa klabu ya Simba SC ya Dar es salaam, Haji Sunday Manara (katikati) akitolewa nje na polisi.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, imempa onyo kali Msemaji wa klabu ya Simba SC ya Dar es salaam, Haji Sunday Manara kwa kosa la kuingia uwanjani.

Kiongozi huyo alifanya kosa hilo Jumapili iliyopita wakati wa mechi ya watani wa jadi ambapo Simba aliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga.

Katika barua hiyo iliyotolewa imemtahadharisha kiongozi huyo kwa kuendelea kufanya matukio mengine kama hayo na endapo ataendelea kamati hiyo itachukua hatua kali za kinidhamu dhidi yake. Soma barua hiyo hapa chini:



  .............................................................................................................

PRETTY KIND Amwangukia Waziri Shonza


Suzan Michael ‘Pretty Kind’
KUTOKANA na hivi karibuni kufungiwa kujihusisha na sanaa kwa miezi sita na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kutokana na kujiachia nusu utupu mitandaoni, msanii wa filamu na muziki, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amemwangukia waziri huyo kwani mambo yanamwendea kombo.


Akipiga stori na Za Motomoto News, Pretty Kind alisema kuwa, kwa sasa yupo kwenye harakati za kuandika barua kwa Waziri Shonza kwa ajili ya kumuomba msamaha, angalau ampunguzie adhabu kwa kuwa amekuwa hohehahe asiyejielewa afanye nini.
“Nimeshaomba sana msamaha na ninaendelea kuomba ambapo kwa sasa ninaandika barua ya kuomba msamaha kwa naibu waziri maana maisha hayaendi,”  alisema Pretty Kind.

..........................................................................................................

Wawili Watupwa Jela Kwa ‘Kumchezea Rafu’ Rais Nkurunziza Katika Mechi


Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza (kulia) akiwa Uwanjani.
Maofisa wawili nchini Burundi wamehukumiwa kwenda jela baada ya Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza kuwashutumu ‘kuchezewa vibaya’ wakati wa mechi ya mpira wa miguu waliyoiandaa.
Rais Pierre Nkurunziza ambaye ni ‘Mlokole’ wa Kanisa la Evangelical Christian amekuwa akitumia muda wake mwingi kusafiri na Timu yake ya Haleluya FC ndani ya Burundi kwa ajili ya kushiriki mechi mbalimbali.
Inadaiwa kuwa Februari 3, Rais huyu na timu yake walicheza na Timu ya mji wa Kaskazini mwa Kiremba.
Kama kawaida, upande wa timu pinzani ulikuwa ukifahamu kuwa unacheza na rais wa nchi na kukubaliana kuwa mchezo utakaochezwa utakuwa mwepesi, na hata kuweza kumruhusu Nkurunziza kufunga goli.
Lakini kutokana na Timu ya Kiremba kuwa na wachezaji wengi ambao ni wakimbizi kutoka Congo ambao hawakujua kama wanacheza na rais wa Burundi, walikuwa “wakimshambulia mara kwa mara anapokuwa na mpira na kumwangusha mara kadhaa”, shuhuda aliwaeleza AFP.
Waliohukumiwa kwenda jela, Juzi Alhamisi ni pamoja na Mratibu wa Kiremba Cyriaque Nkezabahizi na msaidizi wake, Michel Mutama, kwa mujibu wa shirika la habari.
Source: BBC Sports
.............................................................................................................................................................

 Waziri Mwakyembe Amteua Leodeger Tenga Kuwa Mwenyekiti Mpya BMT


Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF), Leodgar Tenga (katikati).
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF), Leodgar Tenga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa(TFF).
Waziri wa Habari Utamaduni wa Michezo, Harison Mwakyembe amethibitisha hilo kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Ijumaa mchana.
Mwakyembe pia amewateua wajumbe sita wa BMT ambao ni Profesa Mkumbwa Mtambo, Beatrice Singano, Kanali Mstaafu Juma Ikangaa,Joseph Ndumbaro,Rehema Madenge na Salmini Kaniki.
Awali, BMT ilikuwa chini ya Dioniz Malinzi ambae uteuzi wake ulisitishwa na Wizara baada ya kutoridhika na utendaji wake.


..........................................................................................................  

Omog: Huyu Okwi ni Mashine


 
Emmanuel Okwi.
KIKOSI cha Simba kilirejea nchini juzi Jumamosi, kikitokea Afrika Kusini kilipokuwa kimepiga kambi kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2017/18, pia Kombe la Shirikisho Afrika.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Simba ambaye ni raia wa Cameroon, Joseph Omog amemmwagia sifa za pekee mshambuliaji wake mpya, Mganda, Emmanuel Okwi kwa kusema kuwa wamelamba dume, kwani mchezaji huyo ni mashine uwanjani.
Akizungumza na Championi Jumatatu muda mfupi tu baada ya kutua nchini, Omog alisema katika muda mfupi ambao amekaa na Okwi katikia kikosi chake amegundua ana mambo mengi ambayo ni tofauti kabisa na wachezaji wengine.
 
“Nashukuru Mungu tumerejea nchini salama lakini pia kambi yetu ilikuwa ni nzuri sana na imetujenga vilivyo kwa ajili ya msimu ujao na imeniwezesha kuwajua vizuri baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni.
“Hata hivyo, nimevutiwa sana na Okwi, kwani katika muda mfupi niliokaa naye kambini nimeweza kugundua mambo mengi kutoka kwake ambayo ni tofauti kabisa na wachezaji wengine.

“Anajua majukumu yake anapokuwa uwanjani, pia nje ya uwanja anajua afanye nini, hakika atakuwa msaada mkubwa kwetu safari hii katika harakati zetu za kuwania ubingwa wa ligi kuu ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika,” alisema Omog na kuongeza:
“Kwa yeyote anayetaka kuthibitisha haya ninayoyasema aje uwanjani siku ya Jumanne (kesho) tutakapopambana na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.”

Sweetbert Lukonge | Dar es Salaam





Comments

Popular posts from this blog