JOTI AJA NA "SANDUKU LA BABU"
MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ akiandaa promo ya "Sanduku la Babu" MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ akiwa kama Amijee MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ akiwa kama Bi Kiboga. MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ ametengeneza filamu inayokwenda kwa jina la Sanduku la Babu. Msanii huyo anajivunia aina ya mfumo aliotumia katika kuandaa sinema hiyo kwa kuirekodi na kushiriki katika nafasi zote pekee yake na kuifanya kuwa filamu sawa na iliyoshirikisha wasanii wengi. Filamu hiyo ambayo inaonekana ni ya maajabu ni kutokana na Teknolojia iliyotumika kwa nafasi zote kuchezwa na mhusika mmoja, ambapo Joti amecheza katika sinema ya Sanduku la Babu kucheza nafasi ya Babu wa Sumbawanga, Bi. Kiboga, Amijee, na kuwashirikisha kidogo wasanii chipukizi. “Nilikuwa nikifikiria sana kuhusu kuingia katika tasnia ya filamu kwani nilitaka kujua baada ya kutengeneza kazi yangu nitaipeleka wapi? Lakini baada ya kukutana na...