WANAHABARI KUMI, WAFANIKIWA KUINGIA FAINALI YA TUZO ZA HABARI ZA UTALII
Frank Leonard alipopata fursa ya kuzungumza na wanahabari wa Arusha wakati wa ziara ya wanahabri wa Iringa jijini humo Jumla ya Waandishi wa Habari 10 wamefanikiwa kufikia hatua ya fainali ya Tuzo za Uandishi wa Habari za Shirika la Hifadhi za Taifa za mwaka 2013. Wanahabari waliofanikiwa kufika hatua ya fainali ni pamoja na Frank Leonard (Habari Leo), Jackson Kalindimya (Nipashe), Humphrey Mgonja (Radio SAUT FM), Raymond Nyamwihula (Star TV) na Vedasto Msungu (ITV). Wengine ni pamoja na Kakuru Msimu (Star TV), Gerald Kitabu (The Guardian), Salome Kitomari (Nipashe), David Rwenyagira (Radio 5) na Cassius Mdami (Channel Ten). Hafla ya utoaji Tuzo za Habari za TANAPA itafanyika siku ya Jumanne tarehe 27 Mei, 2014 jijini Mwanza ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu. Hafla hii itaenda pamoja na Mkutano wa kila mwaka baina ya TANAPA na Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini inay...