HALI YA MZEE MANDELA YAWAACHA MIDOMO WAZI MARAFIKI ZAKE
Mzee Nelson Mandela. Mke wa Nelson Mandela amesema hana wasiwasi na afya ya mumewe kama alivyokuwa wiki moja iliyopita. “Anaendelea kupokea matibabu vizuri,” amesema Graca Machel. Hata hivyo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 94 anaelezwa kuwa katika hali mbaya, ikiwa ni wiki ya tano sasa hospitalini. Juzi Rais Jacob Zuma alisema mpambanaji huyo dhidi ya ubaguzi wa rangi wa watawala wachache weupe wa Afrika Kusini “ameendelea kuwa mpiganaji imara hivi sasa kama ilivyokuwa miaka 50 iliyopita.” Alilazwa tangu Juni 8 kutokana na matatizo ya mapafu. Wiki jana, Zuma alikanusha madai kuwa Mandela hivi sasa hajitambui. Watu wengi ambao wamemwona tangu hapo wamekuwa wakisema anajitambua na ana hisia. BBC imeripoti kuwa Graca amekuwa pembeni mwa kitanda cha Mandela muda wote hospitalini hapo-Medi-Clinic, Pretoria-na amekuwa akijitenga na mgogoro wa kisheria ndani ya familia ya kiongozi huyo ambao umewekwa hadharani katika wiki chache zi...