Posts

Showing posts from January 3, 2014

CHADEMA WAFANYA KIKAO CHA KAMATI KUU LEO JIJINI DAR

Image
   Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa (kushoto) na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed wakati wa Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wajumbe wa Kikao cha Kamati Kuu.

PENNY AKODISHIWA MAMLUKI NA KWENDA KUMSUTA LIVE ... FULL DATA ZIPO HAPA NA MAPICHA YALIVYOKUWA

Image
KATIKA staili ya aina yake ya kuuaga mwaka na kuukaribisha 2014, mtangazaji Peniela Mungilwa ‘Penny’, ambaye ni zilipendwa wa Nasib Abdul ‘Diamond’ alipewa zawadi ikiwemo keki yenye maandishi ya kumsuta. Peniela Mungilwa ‘Penny’. Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano hii nyumbani kwake Mwananyamala Mwinjuma alikohamia hivi karibuni, baada ya watu wanaosadikika kuwa ni wadau wa Wema Sepetu, kufika hapo wakiwa na ‘mzigo’ huo uliojumuisha pia kadi, shampeni na maua. Mmoja wa wapangaji wa nyumba anayoishi Penny, aliliambia gazeti hili kuwa msafara wa magari matatu ulifika hapo na kugonga mlango wakimuulizia mtangazaji huyo wa kituo cha televisheni cha Channel Ten. “Walivyofika sisi tulijua labda leo ni bethidei ya Penny, maana tuliwaona wakiwa na maua, keki, shampeni na kadi, walipomuulizia tukawaambia ametoka, wakaacha mzigo huo wakisema apewe atakaporudi,” alisema shuhuda huyo. Juu ya Keki iliyopelekwa kwa mtangazaji huyo kulikuwa na maandishi yaliyomsut...

Angalia hapa picha hii ndio Sehemu atakapozikwa marehemu dk William Mgimwa kijijini Magunga

Image
Katibu wa mbunge Dr Wiliam Mgimwa Bw Martine Simangwa akiwaonyesha viongozi  wa  CCM eneo ambalo waziri Mgimwa atazikwa  katika  kijiji  cha Magunga kata  ya Maboga  jimbo la Kalenga. ShareThis Copy and Paste

Hatimaye Rose Ndauka apata mtoto wa kike.....

Image
STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amejifungua mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji mwanzoni mwa wiki hii katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar. Akizungumza na Ijumaa, Rose Ndauka alisema anamshukuru sana Mungu kwa kumjaalia kujifungua salama huku mwanaye huyo akiwa na afya njema.   “Ki ukweli kabisa namshukuru sana Mungu kwa zawadi ya mtoto kwa maana nimejifungua salama kabisa,mimi na mtoto tuko vizuri na nafurahi sana kuingia kwenye ulimwengu mwingine kabisa wa cheo kipya cha kuitwa mama,” alisema Rose.   Akasema hivi sasa ataweka shughuli zote pembeni kwa ajili ya kuanza kumlea mtoto mpaka atakapofisha umri ambao anastahili kuachwa ndipo ataendelea na shughuli zake za sanaa.

WARIOBA:SERIKALI TATU SI MZIGO

Image
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, ametetea muundo wa serikali tatu kuwa hauna gharama, tofauti na inavyotafsiriwa na wengi. Mbali na kutetea gharama za uendeshaji wa serikali tatu, Jaji Warioba pia amewashukia wanaodhani mapendekezo ya muundo wa serikali tatu ni yake binafsi, kutokana na msimamo wa siku nyingi wa kiongozi huyo. Akizungumza na Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Jaji Warioba alisema muundo wa serikali tatu umepunguza gharama za uendeshaji. Kwa mujibu wa Jaji Warioba, chini ya muundo huo hata Bunge linatarajiwa kuwa na wabunge 75 tu, hatua ambayo itapunguza gharama. Mwenyekiti huyo alisema kuwa gharama za uendeshaji wa Serikali ya Muungano zitakuwa katika Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mambo ya Nje huku katika maeneo yaliyobaki gharama zake zitakuwa zimepungua zaidi. “Hivi kwa nini hili la muundo wa muungano tunajadili gharama wakati kila mwaka tunapoongeza mikoa, wilaya, tarafa, ...

Serikali yatoa ratiba ya mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa ambaye alifariki juzi akiwa Afrika Kusini

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe.William Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Mazishi ya aliyekuwa waziri wa Fedha Marehemu Dk. William Mgimwa akiongea na waandishi wa Habari jana  jijini Dar es Salaam kuhusu mwili wa marehemu kuwasili tarehe nne saa saba mchana uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere na Shirika la Ndege la Afrika ya Kusini na kuzikwa tarehe sita katika kijiji cha Magunga mkoani Iringa. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya. Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Dk. Florens Turuka (kulia) na Katibu Mkuu wizara ya Afya na Stawi wa Jamii Charles Pallangyo (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe.William Lukuvi (hayupo pichani) Wapigapicha kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimpiga picha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe.William Lukuvi (hayupo pichani)   **** Na Kiza Sungura-MAE...

DK.SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA MIKA 50 YA MAPINDUZI

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kuyafungua Maonesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,yaliyofanyika jana viwanja vya Beit el Ras,katika shamra shamra za sherehe za Mapinduzi,(kushoto) Makamo wa Kwanza wa  Rais Maalim Seif Sharif Hamadi,na (kulia) Makamo wa Pili  wa Rais Balozi Seif Ali Iddi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wananchi katika ufunguzi wa Maonesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,yaliyofanyika jana  viwanja vya Beit el Ras,katika shamra shamra za sherehe za Mapinduzi,(kulia) Makamo wa Pili  wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,pia akiwa mwenyekiti wa maonesho hayo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]  Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamadi,akipokea Sarafu ya Shilingi Hamsini,ya sherehe za Mapinduzi,kutoka kwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya T...

Nay Wamitego - Nakula Ujana (Official Video)

Image

Nay Wamitego - Nakula Ujana (Official Video)

Image

AIBU YA MWAKA MPYA...MUME WA THEA AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU...PICHAZ NA HABARI ZAIDI HAPA...

Image
  MWAKA ulianza vibaya kwa mke wa mtu ambaye jina lake halikupatikana mara moja kumkimbia mumewe na kumfuata mume wa msanii wa filamu, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ aitwaye Michael Sangu ‘Mike’ jambo lililosababisha ale kichapo cha nguvu na kuuanza mwaka mpya vibaya. Tukio hilo lililovuta hisia za wengi, lilitokea siku ya mkesha wa mwaka mpya, usiku wa kuamkia Jumatano, katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ilikuwa ikikonga nyoyo za mashabiki wake. KAMERA ZA IJUMAA Paparazi wetu aliyekuwa ukumbini humo alimuona Mike akiwa upande mwingine na washikaji zake huku wakiendelea kula raha wakati wa shangwe za mwaka mpya wakati mdada huyo ‘kibonge’ akiwa na mumewe na watu wengine wakifanya yao. Ijumaa lilipata shaka kidogo, baada ya kumuona dada huyo akimwacha mumewe kila wimbo unapokolea na kwenda alipokuwa Mike kisha kucheza naye. Harufu ya ugomvi ilianza kunukia mapema, baada ya paparazi wetu ku...

Chege - Chapa Nyingine (Official Video)

Image

KAULI YA ZITTO KABWE BAADA YA MAHAKAMA KUMPA USHINDI DHIDI YA CHADEMA

Image
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana alitinga  mahakama kuu  kupinga kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya Chadema,Kikao ambacho kilikuwa kikutane leo. Hii  ni  kauli  yake  baada  ya  mahakama  kumpa  ushindi; "Jana tulikwenda mahakamani kwa ajili ya jambo moja tu kutaka haki itendeke kwa sababu mahakaama ndiyo chombo cha juu kabisa kwenye nchi yetu cha kuweza kutenda haki mara baada ya kamati kuu ya chama changu kufanya maamuzi ya  kunivua nafasi zangu ambayo niliandikiwa makosa 11 "Nilikata rufaa kwenye baraza kuu la chama ili baraza kuu liweze kuona kama kamati kuu ilifuata taratibu za chama kufikia maamuzi yale japo mimi naamini haijafuata taratibu za chama lakini kwa bahati mbaya viongozi wangu wa chama changu wameamua kuendelea na kikao cha kamati kuu. "Hawajajibu barua yangu ya nia ya kukata rufaa na kuweza kupatiwa taarifa na mwenendo wa kikao ili niweze kukata rufaa kwa mujibu wa c...

MTANDAO WA UNGA WA JACK PATRICK UNATISHA.

Image
BADO habari ya mjini ni skendo ya kunaswa na madawa ya kulevya ‘unga’ inayomtafuna Video Queen wa Bongo, Jacqueline Clifford Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ ambaye inadaiwa kuwa mtandao wake wa biashara hiyo ni wa kutisha, Ijumaa limetonywa. Habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa Jack ambaye aliomba chondechonde asitajwe, alidai kwa sasa vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wamekuwa wakihaha kwa hofu kuwa modo huyo anaweza kuwataja hivyo wanafanya kila linalowezekana ili wamnusuru kama ilivyokuwa kwa Agnes Gerald ‘Masogange’. Ilisemekana kuwa katika mtandao huo, vigogo hao wenye maskani jijini Dar, Rwanda, Uganda, Kenya, Dubai, Thailand, Italia na Hong Kong wamekuwa wakihaha kumuokoa Jack bila mafanikio. “Unajua China siyo rahisi kumchomoa kama ilivyokuwa kwa Masogange (Agness Gerald) aliyenaswa Sauz (Afrika Kusini) kwa sababu wale (China) Tanzania haikuwasaidia kupata uhuru kama ilivyokuwa kwa Sauz. “Ile ngoma ni mbichi, hakuna upenyo wa rushwa...

ZANZIBZR YENYE NEEMA YAJA BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA NJE.

Image
Makamu wa Pili mwa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na uwekezaji katika sekta ya Viwanda, Bandari na Viwanja vya Ndege ya ALTEC hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Balozi Seif akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na uwekezaji katika sekta ya Viwanda, Bandari na Viwanja vya Ndege ya ALTEC Bwana Ramzan Musipov Ofisini kwake vuga Mjini Zanzibar.  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na uwekezaji katika sekta ya Viwanda, Bandari na Viwanja vya Ndege ya ALTEC uliofika ofisini kwake kwa mazungumzo. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na uwekezaji katika sekta ya Viwanda, Bandari na Viwanja vya Ndege ya ALTEC Bwana Ramzan Musipov akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif. (Picha na Hassan Issa wa – OMPR

TAZAMA YALIYOJIRI KWENYE BIRHDAY PARTY YA BABUTALE IKIWEMO NA ZAWADI ALIYOZAWADIWA NA MADEE

Image
Usiku wa kuamkia tarehe 1,meneja wangu Babu tale alikuwa akiadhimisha miaka kadhaa ya kuzaliwa,mimi na team yangu tulitamani tuwepo kwenye sherehe yake lakini bahati mbaya tulikuwa Mtwara kikazi... tunamtakia maisha marefu zaidi,yeye na familia yake..WCB for life Akimlisha keki Dada yangu,Esma Mkubwa Fella akizungumza machache Moja ya suprise kubwa aliyoipata ni pamoja na kuzawadiwa Gari mpya na Madee,BB new model Mda wa kukata keki Madee akimkabidi funguo za Gari Amin akilishwa keki