Posts

Showing posts from June 7, 2017

Halima Mdee na Ester Bulaya Kulipwa nusu Mshahara

Image
Wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) ambao wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge, watalipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana nao kwa miezi kumi. Stahiki hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya Bunge inayosema, “mbunge aliyesimamishwa hataingia tena sehemu yoyote ya ukumbi na maeneo ya Bunge kwa muda wote atakapokuwa amesimamishwa na atalipwa nusu mshahara na nusu posho zinazoambatana na mshahara huo.” Vilevile, kutokana na uamuzi huo wabunge hao watakosa siku 65 za Bunge zinazojumuisha siku 25 zilizobaki za Bunge la bajeti linaloendelea, Bunge la Oktoba na lile la Februari, 2018. Vikao vya mabunge hayo mawili; la Oktoba na Februari kila kimoja huwa na mikutano ya wiki mbili mbili. Wabunge hao walisimamishwa juzi kwa azimio la Bunge licha ya kutokuwapo au kujitetea kutokana na tuhuma zilizokuwa zinawakabili za kudharau kiti cha spika. “Tukutane Bunge lijalo la bajeti,” alisema juzi Spika wa Bunge, Job Ndugai. Bunge l

IGP SIRRO AFANYA ZIARA KIBITI,ATANGAZA VITA KALI,ATANGAZA DONGE LA MILIONI 10 s

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amefanya ziara katika maeneo ya Kibiti na Mkuranga kutimiza ahadi baada ya kuombwa na wazee wa maeneo hayo kufuatia mauaji ambayo yamekuwa yakiripotiwa kutokea mara kwa mara.Mara baada ya kuzungumza na wazee hao, IGP Sirro amesema kuwa wazee hao wametoa ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na namna ya kuwapata waharifu ambao wamekuwa wakifanya mauaji katika maeneo hayo. Sirro amewaahidi wananchi wa maeneo hayo kuwa atatoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa raia mwema atakayetoa taarifa sahihi kwa watu wanaofanya mauaji mkoani. Tazama hapa

MSIBA WA IVAN WAMUIBUA BABA YAKE ZARI,AFUNGUKA MENGI MAZITO

Image
Kwa muda mrefu staa wa muziki na mjasiriamali wa Afrika Mashariki, raia wa nchini Uganda, mwenye maskani yake mengine huko Pretoria, Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amekuwa akionekana Bongo na mama yake mzazi, Halima Hassan hivyo kuibua sintofahamu juu ya alipo baba yake, Hassan Tiale. Hata hivyo, kifo cha mkwe wake yaani aliyekuwa mume wa mwanaye, Zari, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ aliyefariki dunia Mei 25, mwaka huu, kimemaliza utata huo baada ya kumuibua mzee huyo aliyekuwa amejaa tele kwenye msiba huo nchini Uganda. Mzee Hassan alikuwa mmoja wa watu lukuki waliohuzunishwa na kifo cha Ivan ambapo alisema kuwa, alilazimika kuacha shughuli zake ili kuhudhuria msiba huo kwa namna alivyokuwa akiivana na Ivan. “Msiba huu umenigusa sana. Nilipigiwa simu nikiwa Nairobi (Kenya) ambako nilikwenda kumuozesha kijana wangu bibi (mke) “Nilisikia Ivan aliteleza kwa ajili ya presha, akaanguka chini, akachukuliwa, akapelekwa hospitalini Afrika Kusini, akawe

MAREHEMU PHILEMON NDESMBURO AZIKWA MKOANI KILIMANJARO

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Freeman Mbowe akiwasili nyumbani kwa marehemu Philemon Ndesamburo wakati alipohudhuria mazishi yake yaliyofanyika leo  Moshi mkoani Kilimanjaro Marehemu Ndesamburo alifariki wiki iliyopita na kuzikwa leo mkoani humo angalia matukio mbalimbali  katika picha kuhusu tukio zima la ibada ya mazishi.(Picha na Dixonbusagagablog).