Wafahamu Wanawake 4,000 Wanaojifunza Kuwa Maninja Iran

Miongoni mwa wanawake 4,000 wanaochukua mafunzo ya uninja jangwani nchini Iran. WANAWAKE nchini Iran hivi sasa wanajifunza mbinu za wapiganaji wa Ninja kupitia mbinu za Ninjutsu katika klabu ya mafunzo hayo iliyofunguliwa mwaka 1989 iliyopo Jughin, kilomita zipatazo 52 kutoka jiji la Tehran. Mafunzo hayo yanayofanyika jangwani, yamelenga kuwafanya wanawake hao kuwa ākunoichiā, yaani maninja wa kike. Katika mafunzo yao wanawake hao wanafanya mazoezi ya kupanda na kuruka kutoka katika kuta mbalimbali, kujificha katika milima na kuweza ākukataā shingo ya adui bila kelele yoyote.