Posts

Showing posts from September 3, 2017

Mbunge Mteule Viti Maalum CUF, Bi Hindu Mwenda Azikwa

Image
Mwili wa marehemu Mbunge Mteule Viti Maalum Cuf, Hindu Mwenda, aliyefariki nyumbani kwake Kibada Kigamboni ukiwasili makaburi ya Kisutu Dar leo. Maziko yakiendelea. Sheikh (kulia) akifanya  maombi baada mazishi. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) akiwa katika mazishi hayo. …Akiongea  na wanahabari baada ya maziko. HATIMAYE Mbunge Mteule Viti Maalum Cuf, Hindu Mwenda ,  aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Kibada Kigamboni amezikwa leo makaburi ya Kisutu Dar na mamia ya wafuasi wa chama chake na wananchi wengine wa Dar es Salaam. Sheikh aliyeongoza mazishi hayo aliwahimiza wanachama wa Cuf kuendeleza upendo na kufanya kazi kwa ushirikiano ambapo miongoni mwao ni mwenyekiti wa chama hicho anayetembuliwa na Msajili wa Vyama, Profesa Ibrahim Lipumba. Lipumba alimsifia marehemu akisema alikuwa anajituma katika kazi zake na alikuwa mwanachama shupavu na alikuwa mfano kwa wanachama wengine wanaokipenda cha

Uhuru Kenyatta Ampa Onyo Raila Odinga

Image
Aliyekuwa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Aliyekuwa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta a mefunguka na kutoa onyo kwa mpinzani wake Raila Odinga kuwa asahu kuhusu tume mpya ya uchaguzi lakini pia amemtaka Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga kutoingilia kwani wao wameheshimu maamuzi ya mahakama. Uhuru Kenyatta mpinzani wake Raila Odinga (kushoto). Uhuru Kenyatta amesema chama chake cha Jubilee kipo tayari kwa uchaguzi huo wa marudio na sasa wanasubiri Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC iweze kutangaza siku ya uchaguzi na wanaiomba itangaze siku hiyo haraka. Aidha Uhuru Kenyatta amesema kuwa wapinzani hao hawana haja ya uchaguzi bali ni watu ambao wanataka serikali ya mseto kitu ambacho yeye hawezi kukiruhusu hata kidogo Mahakama ya juu nchini Kenya Septemba 1, 2017 ilifuta matokeo ya Urais nchini Kenya na kuamuru kuwa uchaguzi mpya ufanyike katika nafasi ya Urais kutokana na mahakama hiyo kubaini baadhi ya mapungufu wakati wa utoaji wa matokeo hayo ya uchaguz

Waziri Mkuu Majaliwa atoa suluhisho la ajira

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda katika maeneo yao kwani  vitasaidia katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana. Waziri Mkuu alipozungumza na watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro amesema mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda ambao unalenga kuinua uchumi wa Taifa kutoka wa chini kwenda uchumi wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia. “Viwanda hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa vijana kwa sababu vinauwezo wa kuajiri watu wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji wake. Lakini mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda vitawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya kilimo kuwa na tija," Mhe. Majaliwa. Pamoja na hayo Majaliwa ameongeza na kusema kwamba muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo ambalo lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa soko. Ha

Wema Sepetu atupa jiwe gizani

Image
 Malkia wa filamu Bongo , Wema Abraham Sepetu ametupa jiwe gizani ambalo bado halijajulikana ni kwenda kwa mtu gani na kumwambia bado wa kumshusha hajazaliwa kwani yeye alivyo ni majaaliwa kutoka kwa maulana na siyo kujitakia. Wema ametupa jiwe hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuna mtu kamuharibia siku hivyo na kumwambia kwamba yeye hakujitakia kuwa alivyo hivyo mtu huyo ajue kutofautisha. "Wa kunizima hajazaliwa bado jamani... Alafu mjue kutofautisha kati ya Kujaaliwa na kujitakia... Alhamdulillah nyingi kwa Maulana wangu... Sikujitakia... Ni majaaliwa tu... To whom it may Concern... Kuna mtu kajua kuniharibia siku wallah... " Wema Sepetu.  Dongo la Wema mtandaoni Aidha Wema ameongeza kwa kusema katu hawezi kujitutumua kwani anaogopa kujiumiza. Vilevile  tukio hilo linaunganishwa moja kwa moja na mtu ambaye Wema Sepetu amemuhisi anataka kujaribu kudukua mtandao wake wa Instagram hali iliyompelekea kumuandikia ujumbe kuwa katu hatam