Posts

Showing posts from July 10, 2013

RAIS KIKWETE KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA JKT LEO UWANJA WA TAIFA

Image
Picha za matukio mbalimbali za maadhimisho ya jeshi la JKT yaliyofanyika leo jijini dar es salaam  Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea saluti mara baada ya kuwasili Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo tayari kuongoza kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride katika  Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)   Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahoda (kulia) na Mkuu wa JKT Meja Jenerali  Samweli Albert Ndomba (kulia kwake)   katika  Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Baadhi ya askari...

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO- 2013

Image
   Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kuanzia mwaka huu 2013 itaanza mwezi Julai.  Wanafunzi wamepangwa katika shule zenye miundombinu na walimu kwa masomo husika.  Aidha, kama baadae upungufu utajitokeza, wakuu wa shule wameelekezwa kufanya taratibu za kuazima walimu wa muda na kutoa taarifa kwa uongozi wa halmashauri husika kuhusu upungufu wa walimu uliopo.  Kwa nafasi hii, ninaagiza wanafunzi wote kuripoti katika shule walizopangwa tarehe 29 Julai, 2013. Kama kutakuwa na sababu yoyote ya msingi ya kuhamia shule nyingine, uhamisho wa kawaida utafanywa baada ya kuripoti shuleni kupitia kwa mkuu wa shule husika, Mkurugenzi wa Halmashuri/Manispaa na Katibu Tawala wa Mkoa.  ( Wizara haitabadilisha shule walizopangwa wanafunzi) Wanaporipoti wanatakiwa kuwa na:    Original Result slip na Living Cerificate PHILIPO A. MULUGO&(MB)NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 10 Julai, 2013 WASIC...

"NITAENDELEA KUPAMBANA NA WABISHI WASIOTAKA KUHAMA ILI KUPISHA MIRADI YA UJENZI"...MAGUFULI

Image
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ameapa kupambana kwa kuwabomolea au kuwakomesha kwa njia nyingine, watu waliogoma kuhama kwa ajili ya kupisha miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na wizara yake. Katika hilo, tayari amekwishatangaza uamuzi mzito wa kuruhusu kampuni ya ujenzi ya Jaspal Singh, kujenga barabara kwa kiwango cha lami kwa kuzizunguka nyumba za wakazi waliogoma kuhama na kukimbilia mahakamani akiamini kuwa wataondolewa kwa kugongwa na malori yatakayokuwa yakipita baada ya barabara hiyo kukamilika. Pamoja na hilo, Dk. Magufuli amesema atazibomoa bila kulipa fidia nyumba za wananchi nane waliokataa kufanyiwa tathmini ili kupisha mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, endapo hawatabadili msimamo wao huo. Uamuzi huo aliutangaza jana baada ya kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo alibaini kuwa miradi mingi inakwamishwa na wananchi wa maeneo husika. Akiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Kigog...

ZITTO KABWE AWATAKA WANANCHI WAGOME KUILIPA KODI YA SIMU YA SH. 1000.....

Image
AMEDAI KUWA KODI HIYO ILIPITISHWA KINYEMELA Sakata  la  kodi  ya  line  ya  simu  limeendelea  kuwakuna wanasiasa  wetu  ambao  wamekuwa  wakifunguka  kwa  nyakati  mbalimbali  kupitia mitandao  ya  kijamii.... Baada  ya  January  Makamba, Zitto  kabwe  naye  amefunguka  na  kudai  kuwa  kodi  hiyo  ni  batili  na  ilipitishwa  kinyemela  kwa  sababu  ilikuwa  imeshaondolewa.... Huu  ni  ujumbe  wake  aliouweka  katika  account  yake  ya  facebook:   Baada ya  kauli  hiyo,Zitto  Kabwe  aliandamwa  na  maswali  mengi  sana  toka  kwa  wananchi  wakidai  kuwa  "Makamba  alisema  tuwalaumu  ninyi  maana  ninyi  wabunge...

WEMA SEPETU ANASAKWA NA POLISI BAADA YA KUMTUKANA MENEJA WA HOTELI WAKATI POMBE IKIWA UTOSINI

Image
DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo  iliyopo Kawe Beach, jijini Dar. Akizungumza na mwandishi wetu , meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki zake wapatao kumi. Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika  saa tano usiku, Wema na marafiki zake  walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowak era wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo. Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua gl...

HUYO NDO "MELLIS EDWARD" ALIYEKAMTWA NA MADAWA YA KULEVYA AKIWA NA "AGNESS MASOGANGE

Image
Picha  ya  Mrembo Mellis Edward  aliyedakwa  na  madawa  ya  kulevya  Afrika  kusini  akiwa  na  Agness Masogange Mellis Edward Inahisiwa kuwa  huyu mwanamke wa pili aliyetajwa na Kamanda Nzowa kwa jina la “Melisa Edward”   ni mdogo wake na Agnes ambaye katika akaunti ya facebook anayo tumia jina la (MELLIS EDWARD) , Agnes amemuweka katika orodha ya family kama ‘sister’ katika akaunti yake ya Facebook.  Kamanda  Gofrey  Nzowa - Kitengo  cha  Madawa ya Kulevya   Agness Masogange  akiyahesabu  "MAPESA" yake.Picha  hii aliiweka  siku  chache  zilizopita

CHADEMA YAJIPANGA KUIMARISHA KITENGO CHA ULINZI NA USALAMA " RED BRIGADE" ILI KUWAKABILI VIJANA WA CCM WATAKAOLETA FUJO

Image
MUHTASARI Ili kukabiliana na vitendo vya fujo vinavyofanywa na vijana wa CCM dhidi ya wagombea, Wanachama na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama “Red Brigade” kiimarishwe zaidi kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi nzima wanapewa mafunzo maalum ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi maalum katika mikoa yote.  RIPOTI  KAMILI TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA KILICHOFANYIKA TAREHE 06-07/07/2013 KATIKA HOTEL YA BLUE PEARL, DAR ES SALAAM. Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ilikutana katika Kikao cha dharura kuanzia tarehe 06-07/07/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Dar es salaam kujadili pamoja na mambo mengine Rasimu ya Katiba mpya na hali ya Siasa nchini. Kamati kuu imejadili na kuyatolea maamuzi mambo mbalimbali kama ifuatavyo: 1:0. Hali ya Siasa Nchini. Kamati kuu imepokea taarifa ya hali ya siasa nchini na kuzingatia mambo yafuatayo: a)...

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZA LAANA ZA KUNDI LA BAIKOKO - TANGA

Image
Hizi  ni  baadhi  ya  picha  za  kundi  la  wacheza  uchi / nusu  uchi  maarufu  kwa  jina  la  Baikoko  lenye  maskani  yake Tanga....   Ndugu mtazamaji wetu ukiwa kama ni mtanzania mwenye maadili ya kitanzania ,Je! kweli huu ndo utamaduni tulilofundishwa?       TUPE MAONI YAKO?

"NASUBIRI WAKATI MWAFAKA WA KUMUONYESHA KIKWETE YA KWAMBA MIMI NI NANI".....HILI NI TISHIO LA KIHUNI LA RAISI KAGAME WA RAIS KIKWETE

Image
Nikiwa  katika  upekuzi  wangu, nimeshtushwa sana na kauli za  KIHUNI  za Rais  Paul Kagame  dhidi ya  Rais wetu Kikwete na nchi yetu kwa ujumla.... Rais Kikwete ameepuka malumbano na Kagame kwa  kukaa  kimya , lakini inaelekea Kagame  anadhani ukimya wa Kikwete ni uoga kwake  au labda anatafsiri kuwa anadharauliwa..... Nadhani  huu  ni  wakati  mwafaka  kwetu  sisi  watanzania  kuungana  na  kumuunga  mkono  rais  wetu  juu  ya  huu  UPUMBAVU  wa  Kagame.... Kagame  ni  lazima  atambue  kwamba  watanzania  tupo  tayari  kuilinda  nchi  yetu  kwa  gharama  yoyote  na  kamwe  hatuwezi  kuwa  VIBARKA  wa  Rwanda... Ifuatayo  ni  Kauli  ya  Kihuni  aliyoitoa  Rais  Kagame  Kwa...