Posts

Showing posts from April 2, 2017

Mjane mwingine aibukia wanahabari na Zigo la nyaraka

Image
Mjane Farida Saleh Amrani amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kulalamika kudhulumiwa nyumba yake aliyoachiwa na marehemu mme wake aliyefariki mwaka 2011. Akizungumza na kuonesha hati halali za nyumba hiyo yenye kitalu namba 2111 iliyopo Mbezi Beach Kata ya Maliasili, Farida alisema kuwa katika nyumba hiyo walihamia mwaka 2002 na hati ya nyumba hiyo ilikuwa kwa mwanasheria kipindi chote hata pale marehemu mumewe alipofariki. Amesema kuwa, baada ya mume wake kufariki mtoto wa marehemu mkubwa aliambiwa afungue mirathi lakini akawa anasema taratibu za kabila la kihaya ni baada ya mwaka mmoja kumalizika. Farida ameeleza kuwa, mumewe Alfred Kyoma alifariki akiwa safarini Bukoba na amemuacha na watoto wawili ambao baada ya kumalizika kwa msiba familia nzima walikubaliana nyumba ipangishwe ili fedha zitakazopatikana ziwasomeshe watoto,ambao mmoja yupo kidato cha tano sasa hivi na mwingine cha kwanza. Nyumba hiyo kwa Yusuph Shaban Omari ambaye ni mmiliki

Mh! kwa Nape Hapana!- UWOYA

Image
IRENE Uwoya amekataa katakata kuzungumzia chochote kuhusiana na kutumbuliwa kwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye na kusema chochote ambacho kipo, kiendelee kubaki hivyo hivyo lakini kwa upande wake ameziba mdomo. Gazeti hili lilikuwa likimtaka Uwoya kuzungumzia kuachwa kwa waziri huyo katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yaliyofanywa hivi karibuni na Rais Dk. John Pombe Magufuli na nini mtazamo wake kwa waziri mteule, Harrison Mwakyembe, lakini muigizaji huyo alikataa katakata. “Jamani mimi kwenye hilo sitaki kuzungumzia chochote jamani mambo ya siasa mimi hapana kwa sasa kilichopo ndicho kiendelee hivyohivyo,” alisema Uwoya.

Dkt Mwele Aliyetumbuliwa na JPM, achukuliwa umoja wa mataifa

Image
Dkt. Mwele Malecela aliyekuwa Mwanamke wa kwanza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR na kisha 'kutumbuliwa' baada ya kutangaza uwepo wa homa ya Zika nchini, sasa anakuwa Mkurugenzi wa Vituo vya kuzuia na kudhibiti magonjwa Afrika wa Umoja wa Mataifa (WHO-AfRO) Mwele alipata kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu(NIMR), baadae uteuzi wake ulitenguliwa.

KAIRUKI: SERIKALI HAITAMVUMILIA MTUMISHI MWENYE VYETI FEKI

Image
Inakadiriwa kuwa watumishi 4,300 wapya wanataajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu na wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja baada ya kukamilika kwa zoezi zima la kuhakiki watumishi hewa.Hayo yamebainishwa mkoani Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Mh. Angela Kairuki, wakati akizungumza na watumishi na wanachuo, ambapo amesema kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya watumishi hewa huku likipoteza fedha nyingi.Aidha Mhe. Kairuki amesema kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye atabainika kuwa na vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua madhara ya vyeti hivyo kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki.Amewataka wahitimu katika kada mbali mbali kutowaonea haya watu ambao wanataka kupora ajira za wenzao.

RAIS MAGUFULI: OLE WAKE ATAKAYEIZUIA KAMATI YA KUCHUNGUZA MCHANGA WA DHAHABU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 01 Aprili, 2017 aliwaapisha wajumbe wa kamati maalum ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Hafla ya kiapo kwa wajumbe wa kamati hiyo imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Harold Nsekela na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama. Kamati hiyo ya wanasayansi 8 walioteuliwa na Mhe. Rais Magufuli tarehe 29 Machi, 2017 inaongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Abdulkarim Hamis Mruma na itafanya kazi ya uchunguzi kwa siku 20 kisha kuwasilisha ripoti yake kwa Mhe. Rais. Akizungumza baada ya kuwaapisha, Mhe. Rais Magufuli amesema ameamua kuunda kamati hiyo yenye wasomi waliobobea katika