Posts

Showing posts from July 28, 2017

Alichokisema John Mnyika baada ya Spika kubariki kufutwa uanachama Wabunge 8 wa CUF

Image
Mbunge wa Kibamba John Mnyika leo July 28, 2017 ameielezea hatua ya Spika Ndugai kubariki kufutiwa uanachama Wabunge wa Viti Maalumu wa CUF akisema ni makosa kwa kuwa kuna kesi Mahakamani kuhusu utata wa uongozi wa Chama hicho. Aidha, Mnyika amemuomba Spika kutangaza wateule ambao wametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi July 27, 2017 kuwa hawataapishwa mpaka mashauri yao yaliyopo Mahakamani yamalizike. Hatua ya John Mnyika imekuja siku chache baada ya Spika kuridhia kufutiwa uanachama Wabunge wanane wa CUF baada ya kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wake Prof. Lipumba kisha kutangaza nafasi zao kuwa wazi na kumuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya taratibu zilizostahili ambapo alitangaza majina ya Wabunge wengine wanane kuziba nafasi zao.

NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA UBUNGO

Image
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakisoma muongozo. Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo anapenda kuwatangazia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa Kama ifuatavyo:- Msaidizi wa Hesabu Daraja la II X 3 SIFA: Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambulikajja Serikali au Cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA. KAZI NAMAJUKUMU: i)Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu. ii) Kutunza kurnbukurnbu zahesabu. iii) Kupeleka barua/nyaraka za Uhasibu benki. iv) Kufanya Kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu NGAZI YA MSHAHARA – TGS.B -Shilingi 390,000/- MASHARTI YA JUMLA: • Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania, • Awe amehitimu na Kupata Cheti cha Taaluma cha kidato cha Nne (IV) NB. Results Slip hazikubaliki • A...

Shaffih Dauda ajitoa kugombea TFF

Image
Shaffih Dauda. Mtangazaji wa Clouds Media Group, Shaffih Dauda ametangaza kujitoa rasmi katika kinyang’anyiro cha kuwania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatia tuhuma za rushwa zinazomkabili. Shaffih ambaye ni mmoja wa wachambuzi maarufu wa soka nchini ametangaza uamuzi huo mapema leo asubuhi Julai 28 wakati akizungumza kupitia kipind cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv. Akieleza sababu za uamuzi huo, Shaffih amesema kuwa imekuwa ni kazi ngumu ya miaka mingi kuweza kulijenga jina lake hadi kufikia hapo alipo leo, hivyo hawezi kuacha tuhuma hizo za rushwa zinazomkabili sababu ya uchaguzi wa TFF ziendelee kumchafua. “Nimetumia muda mrefu kujenga brand yangu hakuna haja kuendelea kung’ang’ania. Suala la Rushwa ni kunichafua na mimi sitaki,” alisema Shaffih. Uamuzi huu umekuja ikiwa ni siku chache tu tangu alipokamatwa na kuhojiwa na TAKUKURU yeye na wenzake kwa tuhuma za kupanga kufanya vitendo vya rushwa jambo amb...

Breaking News: Mfanyakazi wa Acacia Akamatwa Airport Dar Akiondoka Nchini

Image
Kampuni ya Acacia imesema kuwa mmoja wa wafanyakazi wake wa kimataifa anayefanya kazi na Pangea Minerals Limited amezuiwa kuondoka Tanzania leo Julai 28 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya asubuhi. Acacia wameeleza kuwa, mfanyakazi huyo ambaye hawakumtaja jina alikamatwa na hati yake ya kusafiria ilichukuliwa huku na yeye akishikiliwa kwa muda. Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya kampuni hiyo, Acacia wamedai kuwa baada ya kuingilia sakata hilo kisheria, mfanyakazi huyo aliachiwa na hati yake ya kusafiria ikarejeshwa. Aidha, wamesema tukio hilo limetokea kipindi ambacho kwa takribani siku mbili sasa wafanyakazi wake wamekuwa wakisumbuliwa na maafisa mbalimbali wa serikali. Kuhusu tuhuma hizo, serikali kupitia kuwa Msemaji Mkuu, Hassab Abas imesema kuwa inafuatilia tuhuma hizo na baada ya muda mfupi watatoa taarifa kamili. “Tunafuatilia ukweli wa madai ya Acacia kuwa mmoja wa maafisa wake amezuiwa kuondoka T...

Mke wa Mugabe amtaka mumewe kumtangaza mrithi

Image
Rais Mugabe na mkewe bi Grace Mugabe Rais wa Zimabwe ametakiwa na mkewe kumtaja ''mrithi'' wake ili kupunguza migawanyiko kuhusu mtu atakayemrithi. ''Rais hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno alke litakuwa la mwisho'',alisema bi Grace Mugabe. Bwana Mugabe ndio kiongozi mzee zaidi na chama chake cha ZANU PF kimemchagua kuwania urais kwa mara nyengine mwaka ujao. Lakini makundi pinzani yamekuwa yakiwania urais ili kuimarisha uwezo wao huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.

KESI YA AKINA RUGEMALIRA NA SINGASINGA YAAHIRISHWA

Image
James Rugemalira (mwenye mvi) na mwenzake  Harbinder  Singh Sethi wakifikishwa mahakani. MAHAKAMA  ya  Hakimu Mkazi Kisutu  leo imeahirisha kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya  IPTL, Harbinder  Singh Sethi  maarufu kama  ‘Singasinga’   na  mfanyabiashara  James Rugemalira wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara. Rugemalira na Harbinder Singh Sethi baada ya kutoka kortini. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 3 mwaka huu, mbele ya  Hakimu Mkazi Mkuu ,  Huruma Shaidi  baada ya wakili wa serikali, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Ester Bulaya Ambwaga Tena Wasira Kortini

Image
Ester Bulaya. Mahakama ya Rufani imetupilia mbali rufaa dhidi ya Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) . Hukumu ya rufaa hiyo imesomwa leo Julai 28 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Elizabeth Mkwizu. Wapiga kura hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walikata rufaa mahakamani hapo wakipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, iliyompa ushindi Bulaya katika kesi ya uchaguzi waliyoifungua wakipinga matokeo yaliyompa ushindi Bulaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 dhidi ya Steven Wasira (CCM) .   Wasira . Rufaa hiyo ilisikilizwa Mei 11 mwaka huu na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani. Akisoma hukumu hiyo Naibu Msajili Mkwizu amesema kuwa hoja za warufani hao hazina msingi kwani kasoro walizokuwa wakizilalamikia hazikuwa na athari katika matokeo ya uchaguzi huo.