Posts

Showing posts from March 31, 2017

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ALIYEWASILI MCHANA HUU JIJINI DAR

Image
Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa. Imeelezwa kuwa ujio wa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia ni pamoja na kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja ‎na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.Mhe. Dessalegn atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mazungumzo na kushuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari. Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake ,Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn,aliyewasili hivi punde katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar Es Salaam.   Waziri

HIVI NDIVYO "BOMBARDIER" ZA ATCL ZILIVYOKUSANYA BILIONI 9 KWA MIEZI MINNE TU

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.  Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100. KUMBUKUMBU: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa n

TANZIA: MBUNGE DKT. ELLY MARKO MACHA AFARIKI DUNIA

Image

KESI YA MALKIA WA MENO YA TEMBO KUSIKILIZWA TENA WIKI IJAYO

Image
Kesi inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan (66) maarufu kama Malkia wa tembo inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam itaendelea kusikilizwa kuanzia Aprili 5 hadi 7, mwaka huu. Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba mawakili wanaosikiliza kesi hiyo hawapo. Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Hassan Kiangio alidai kuwa kesi hiyo imeahirishwa kwa mara ya pili tangu mshitakiwa Manase Philemon (39) kudai amepigwa na kuteswa wakati akichukuliwa maelezo yake, ambapo upande wa mashitaka ulitakiwa kuleta mashahidi ili kuthibitisha tuhuma hizo. Hatua ya upande wa mashitaka kuleta mashahidi ni kusikiliza kesi ndogo ndani ya kesi kubwa baada ya shahidi Sajenti Beatus (46) kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kudai kuwa aliandika maelezo ya mshitakiwa huyo na baadaye mshitakiwa kupinga kupokelewa kw

Utata waibuka malori ya mafuta yaliyoibwa Arusha

Image
Arusha. Utata waghubika kuibwa na kupatikana kwa magari mawili ya mafuta mali ya Kampuni ya Mount Meru. Taarifa za kuibwa kwa magari hayo mkoani Arusha yakiwa na mafuta aina ya dizeli lita 77, 000 na kupatikana siku ya pili yakiwa wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro zinaelekeza kuwa kamera maalumu za (CCTV) ziliondolewa sehemu yalipokuwa yameegeshwa magari hayo. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate, Eliuta Mwanjawike alisema kampuni yao baada ya kupata taarifa ya kuibwa magari hayo na walinzi wake wawili, waliunda kamati ya uchunguzi iliyobaini upungufu ukiwapo wa tofauti ya taarifa kati ya meneja mkuu wa kampuni hiyo na mkurugenzi. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Irembo alikiri kupata taarifa za magari hayo kuibwa na kudai kuwa wameamua kuyaondoa eneo la polisi. “Magari hayo tumemkabidhi mmiliki kwa sababu yalikuwa na mafuta mengi na tusingeweza kukaa nayo hapa ila kesi ikishafika mahakamani basi yataletwa hapa,” alisema Yusuph. Mkurugenz