Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hammad (kushoto) akiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuno na Uzima, Askofu Josephat Gwajima. LEO Mei 10, 2017, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hammad amekwenda kumtembelea Mchungaji wa Kanisa la Ufufuno na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, kanisani kwake Ubungo, Dar es Salaam. Akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo ya faragha na Maalim Seif, Askofu Gwajima amesema ujio wa kiongozi huyo kanisani hapo ulikuwa ni kwa ajili ya kubadilishana mambo mbalimbali kuhusu nchi na mahusiano yao. “Maalim Seif ni rafiki yangu, ni siku nyingi tulikuwa hatujaonana, tumezungumzia mambo ya nchi mbalimbali na mahusiano yangu mimi na yeye. “Unaweza kuwa na rafiki ambaye anafanya kazi tofauti na yako, anaweza kuwa daktari na wewe ukawa siyo daktari, hata serikali haikatazi urafiki. “Nimemuuliza ni kipi kimempata Profesa (Lipumba) mpaka anavuruga chama chake, amenielezea ili na...