Posts

Showing posts from May 21, 2017

KULIKONI !? Sumaye Kujiuzulu ujumbe wa bodi CRDB, KISA?!

Image
Waziri Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Mashariki, Frederick Sumaye, amejiuzulu ujumbe wa bodi ya Benki ya CRDB ili atekeleze zaidi majukumu yake ya kisiasa. "Nina shughuli nyingi za kisiasa ambazo zitaninyima nafasi ya kuhudhuria vikao vya bodi.  Sipendi pia kuona CRDB ikihusishwa na msimamo wangu kisiasa. Hii ni taasisi huru ambayo ina wanahisa wengi ambao sitapenda kuona maslahi yao yakiingiliwa kutokana na siasa,"  amesema Sumaye.

Uthibitisho wa Simba kufika FIFA

Image
Ushahidi kuwa klabu ya Simba imewasilisha malalamiko yake kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), umepatikana. Kitendo cha Simba kuwasilisha rufaa hiyo na picha ikionyesha ushahidi huo, inaonekana kuwakwaza zaidi ya mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wameanza sherehe za ubingwa. Baadhi ya mashabiki wa Yanga, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwaita Simba “Wazee wa pointi za mezani”. Lakini mashabiki wa Simba wamekuwa wakijibu mapigo na kusema, “Haki ni haki” na sheria itafuata mkondo wake. Yanga na Simba zimemaliza ligi zikiwa na pointi 68 kila moja, lakini Yanga ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa GD. Silaha ya Simba, inabaki kuwa suala la pointi za Kagera na kama kweli Fifa itaamuru irejeshewe, basi itafikisha pointi 71 na kutangazwa kuwa bingwa. Simba ilishinda rufaa yake kupitia kamati ya Saa 72 ambayo ilibaini kuwa kweli beki Mohammed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano wakati Simba ilipolala kwa mabao 2-1 katika mechi ya ligi...

WATANZANIA 11 WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMBAKA KWA ZAMU MAMA MJAMZITO AFRIKA KUSINI

Image
Wanaume 11 ambao ni raia wa Tanzania wamekamatwa na Polisi na kufikishwa Mahakamani wiki hii Johannesburg Afrika Kusini .Radioni na Mtandaoni Johannesburg wiki hii kumeripotiwa kuwa kosa lililofanya Wanaume hao 11 kukamatwa na Polisi ni kumbaka Mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 22 aliyekuwa akitoka kazini saa kumi na moja alfajiri.Mwanamke huyo alikuwa akitoka kazini na Mfanyakazi mwenzake ambaye ni Mwanaume ambapo ghafla walivamiwa na kundi la Wanaume wenye silaha za moto na wakamvuta Mwanamke huyo kabla ya kumpiga Mfanyakazi mwenzake ambae baadae alifanikiwa kutoroka.Baada ya Mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu Polisi na wakafanikiwa kuwahi eneo la tukio na kukuta Wanaume hao wakimbaka kwa zamu Mwanamke huyo mwenye ujauzito wa miezi mitatu.Polisi wapatao kumi waliingia kwenye jengo tukio lilikofanyika na kumuokoa Mwanamke huyo aliyekua kwenye hali mbaya ambapo walimpeka Hospitali huku Watuhumiwa wakichukuliwa na kupandishwa Mahakamani siku ya Jumatano. ...

Dalili za Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo

Image
Hapo kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo, kisha tukasoma kuhusu dawa mbadala ya vidonda vya tumbo, tukasoma tena kuhusu chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo, na leo tunaendelea kuangalia dalili za ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na; Kuchoka choka sana bila sababu maalum Kuuma mgongo au kiuno Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia Kizunguzungu Kukosa usingizi Usingizi wa mara kwa mara Maumivu makali sehemu ya mwili Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali. Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali Kichefuchefu Kiungulia Tumbo kujaa gesi Tumbo kuwaka moto Maumivu makali sehemu kilipo kidonda Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi Kutapika nyongo Kutapika damu au kuharisha Sehemu za mwili kupata ganzi Kukosa hamu ya k...

WACHIMBAJI WA MADINI WAFARIKI KWA KUKOSA HEWA MGODINI TANZANIA

Image
Wachimbaji wawili wadogo wa madini ya dhahabu katika kijiji cha Masuluti kata ya Magulilwa tarafa ya Mlowa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefariki dunia baada ya kukosa hewa. Wananchi wa Msuluti kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa wakiwa wamebeba mmoja kati ya miili ya wachimbaji wadogo wawili waliokufa mgodini kwa kukosa hewa leo Miili ya wachimbaji wadogo wawili katika mgodi ya Mamweli Msigwa ukiingizwa kwenye gari la polisi Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi katikati mwenye kofia nyeusi akionyeshwa shimo la mdogi wa dhahabu ambalo limesababisha vifo vya watu wawili Wananchi wakiwa eneo la tukio Askari polisi na wananchi wakitazama mgodi huo uliouwa Milili ya wachimbaji wadogo wawili walipoteza maisha mgodini leo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi kushoto akitazama shimo la mgodi katika kijiji cha Msuluti kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa ambalo wachimbaji wawili wadogo wawili walipoteza maisha kwa kukos...

BIZARI: KIUNGO CHA MBOGA CHENYE FAIDA NYINGI

Image
Inawezekana katika maisha yako hujawahi kula mboga iliyowekwa kiungo kinachoitwa bizari, kama umewahi, inawezekana pia hujawahi kujua faida zake mwilini. Bizari (Turmeric) ni kiungo cha mboga jamii ya mimea unaochimbwa kama mizizi, mfano wa tangawizi, lakini tangawizi yenyewe ina rangi ya njano na hujulikana pia kama ‘manjano’ kutokana na rangi yake. Kiungo hiki kinatumiwa sana katika Bara la Asia na hasa India na China. Kutokana na umuhimu wake kiafya, vyakula vingi hupikwa kwa kuchanganya na kiungo hiki ambacho sasa kimeenea dunia nzima, ikiwemo Tanzania. FAIDA ZA BIZARI KIAFYA Bizari hutumika na watu wengi kama kiungo cha mboga cha kuongeza ladha katika mchuzi na pengine kuweka rangi, lakini kuna faida nyingi unazozipata unapotumia kiungo hiki kila mara katika mapishi yako. Inaelezwa kuwa bizari ina virutubisho vyenye uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili, mara 8 zaidi ya Vitamin C na Vitamin E, ina uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu (cholesterol) na kuzuia...

WACHEZAJI WA RUVU SHOOTING WAPATA AJALI SINGIDA

Image
Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba msafara wa timu ya Ruvu Shooting umepata ajali mbele kidogo ya Singida wakiwa safarini kurejea nyumbani.Taarifa kutoka kwa mmoja wachezaji waliokuwapo inasema kwamba gari likiwa katika mwendo tairi lilipasuka na kusababisha gari kuhama njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.Hakuna mtu yoyote aliyeumia sana japo kuna mchezaji mmoja ambaye amepata majeraha ya kawaida. Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde....

Rais Magufuli akabidhi rasmi uenyekiti EAC kwa Rais Museveni

Image
Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo (Jumamosi) amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni. Muda mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia madarakani. “Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka jana. Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake. “Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema. Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu na uwezo wake wote.