Kafulila afunguka haya kuhusu Escrow
DAR ES SALAAM: WAKATI gumzo nchi nzima likiwa ni wizi mkubwa ambao haujawahi kufanyika wa zaidi ya shilingi bilioni 300 kutoka akaunti iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Tegeta Escrow, imeelezwa kuwa baadhi ya wabunge walikuwa wakihatarisha maisha yao na wengine wamepoteza ubunge kwa sababu ya kupinga ufisadi huo. Vinara wa kufichua sakata hilo, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ndiyo waliofichua mambo hayo kwa nyakati tofauti. Kafulila aliyehojiwa na gazeti hili wiki iliyopita alisema kundi lao la kupiga vita ufisadi huo lilikuwa hatarini kwa sababu kuna fedha zilikuwa zinatumika ili kuzima wizi huo. Marehemu Deo Filikunjombe (ushoto), Davidi Kafulila, Zitto Kabwe pamoja na David Silinde. “Hata wenzetu wabunge walikuwa wakitupinga na kwa kweli tulikuwa katika wakati mgumu, hata hivyo, hatukuacha kupigania jasho la umma ambalo lilikuwa limeliwa na watu wachache,” alisema Kafulila. Alisem...