Posts

Showing posts from May 4, 2016

BREAKING NEWS : SNURA AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA SANAA,VIDEO YA CHURA YATAKIWA KUFUTWA MTANDAONI

Image
 snura katika pozi Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla akiongea na waandishi wa habari Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa. Pia imeufungia wimbo wake Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye redio na TV nchini. Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar. Uamuzi wa kumfungia umekuja kutokana msanii huyo kutojisajili kwenye Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA.

Sumaye Amkejeli Rais Magufuli kwa kazi anayofanya

Image
FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na kuchukia kukosolewa Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli ameleza kushangazwa na hatua ya serikali kuminya uhuru wa habari na kwamba, kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu yanayofanywa na watendaji wake.   “Wapowatawala ambao hawapendi kusemwa lakini wanapenda sana kusifiwa. Kiongozi mwenye tabia ya udikteta hataki kusikia kingine zaidi ya sifa zake tu.   “Huyo ni mtu hatari na katika nchi ya namna hiyo hakuna uhuru wa habari wala uhuru wa kutoa maoni kwa woga wa kupotezwa kusikojulikana,” amesema Sumaye. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoratibiwa na Cha

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI DODOMA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. K

Mwili wa Papa Wemba Wawasili DRC

Image
Kinshasa, Kongo Mamia ya watu wamekusanyika leo nje ya Uwanja wa Ndege wa Kinshasa nchini Kongo wakisubiri mwili wa mwanamuziki aliyefariki Jumapili iliyopita, Papa Wemba kuwasili nchini humo. Zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Papa Wemba litafanyika wiki ijayo Jumatatu katika uwanja wa Kinshasa, DRC ambapo mashabiki wake pamoja na raia wote watatoa heshima zao za mwisho kwa mwanamuziki huyo. Papa ambaye amefariki makiwa na umri wa miaka 66, ametajwa kuwa mmoja watu waliokuwa na ushawishi mkubwa Afrika ya Mashariki na kwamba ni miongoni mwa waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne ijayo baada ya kuagwa Jumatatu. Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini Abidjan ambapo mwanamuziki huyo alianguka alipokuwa akiimba. Mwanahabari

Kangi Lugola Afurahia Sefue Kutumbuliwa…..Ataka Majipu Sugu Wizara ya Kilimo Yaliyoota Sehemu Nyeti Yatumbuliwe

Image
Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola jana alichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa hisia kali huku akimpongeza Rais John Magufuli kwa kumtumbua Katibu Mkuu Kiongozi. Ingawa hakumtaja kwa jina, Balozi Ombeni Sefue ndiye Katibu Mkuu Kiongozi aliyeondolewa na Rais Magufuli Machi mwaka huu bila kubainisha sababu ikielezwa kwamba angepangiwa kazi nyingine. Lugola alisema Rais Magufuli ameonyesha kwa vitendo kuwa anamuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kauli yake kuwa Ikulu ni mahali patakatifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba. Lugola alisema kwa kuwa alikuwa akichangia kwa mara ya kwanza bajeti ya Serikali ya Awamu ya Tano, ni vyema akampongeza Rais kwa namna anavyotumbua majipu kwa ujasiri na bila kupepesa macho. Lugola akirejea kauli inayosema “kama unataka mali utaipata shambani”, alimtaka Waziri Nchemba kutumbua majipu katika wizara yake.

UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO SIRI YA MAFANIKIO BARA LA AFRIKA – NDUGAI

Image
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika. Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika. Spika wa Mhe. Job Ndugai akiwa na baadhi ya Maspika wenzie kutoka mabunge ya Nchi za Bara la Afrika kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament) alikoalikwa kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa B