SUMAYE AIANGUKIA SERIKALI WANANCHI KUVAMIA SHAMBA LAKE LA EKARI 33 MABWEPANDE
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kuwasili eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kuangalia eneo la ekari 33 la Sumaye lililovamiwa na wananchi. WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (wa pili kulia), na mke wake mama Esther (kushoto), wakimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia) eneo la shamba lake la ekari 33 lililopo Mabwepande Manispaa ya Kinondoni lililovamiwa na wananchi walipotembea eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi. Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo. DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe. Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake. Mhe. Sumaye akielezea uhalali wake wa kumiliki eneo hilo. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya, Justine Chiganga...